KUTEMBEA KATIKA ROHO-3
KUTEMBEA KATIKA ROHO-3
Bwana Yesu asifiwe sana mwana wa
Mungu..!!
Karibu sana tuendelee na sehemu
ya tatu ya Mwendelezo wa somo letu la KUTEMBEA KATIKA ROHO,kama hukupata nafasi
ya kupitia sehemu ya kwanza,na ya pili unaweza kulipata kwenye blog yetu ya
rhemavoice.blogspot.com au kwenye page yetu ya facebook-Rhema’s
Voice Ministry.
Sehemu ya pili tuliomwangalia
Mtumishi wa Mungu Musa, leo tunaendelea kwa kumwangalia Mtumish wa Mungu
Ahithofeli
2.Ahithofeli.
Huyu ndugu sio mtu maarufu sana
kwenye Biblia lakini alikuwa mtu muhimu sana katika mafanikio ya Mfalme
Daudi.Huwezi kuzungumzia Mafanikio ya Ufalme wa Daudi bila kumtaja huyu
ndugu.Katika moja ya watu ambao Mungu alimpa Daudi ni huyu ndugu Ahithofeli.Alikuwa
na Karama ya Ajabu,Shauri lilitoka kinywani mwake lilikuwa kana kwamba limetoka
moja kwa moja kwenye kinywa cha Mungu mwenyewe.Alikuwepo Kuanzia utawala wa Daudi
mpaka utawala wa Absolum mtoto wa Daudi.
Tutazame maandiko
2Samweli 16:20-23
20 Kisha Absalomu akamwambia
Ahithofeli, Haya, toa shauri lako, tufanyeje.
21 Naye Ahithofeli akamwambia
Absalomu, Ingia wewe kwa masuria ya baba yako, hao aliowaacha ili kutunza
nyumba; na Israeli wote watasikia ya kuwa umechukizwa kabisa na baba yako;
ndipo itatiwa nguvu mikono yao wote walio pamoja nawe.
22 Basi wakamtandikia Absalomu hema
juu ya nyumba darini; naye Absalomu akaingia kwa masuria ya babaye machoni pa
Israeli wote.
23 Na shauri lake Ahithofeli,
alilokuwa akilitoa siku zile, lilikuwa kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu;
ndivyo yalivyokuwa mashauri yote ya Ahithofeli, kwa Daudi, na kwa Absalomu.
Mstari wa 23 unasema katika
kipindi cha Daudi na Absalomu Shauri lililotoka kinywani mwa huyu mtumshi
lilikuwa kama Neno litokalo kinywani mwa Bwana.
Ukiona hata hapo juu Absalomu
alipoomba shauri kipindi amempindua Baba yake Daudi huyu jamaa alitoa Shauri
sawasawa na Adhabu aliyoisema Bwana kwa Kinywa cha Nabii Nathani kipindi Daudi
alipodhini na mke wa Huria.Msikie Nabii Nathani hapo mwanzo
2Samweli 12;11-12
11 Bwana asema hivi, Angalia,
nitakuondokeshea uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya
macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako mbele ya jua hili.
12 Maana wewe ulifanya jambo lile
kwa siri; bali mimi nitalifanya jambo hili mbele ya Israeli wote na mbele ya
jua.
Tazama Mungu alisema Neno hili
kipindi Daudi amekosa na hapa Absalomu anaingia tu madarakani anauliza Shauri
kwa Ahithofeli na Shauri analopewa ni Neno lilelile lilotamkwa na Nabii
Nathani.
Pamoja na Kuwa Huduma kubwa hivi
huyu ndugu mwisho wake haukuwa mzuri hata kidogo na hii ni kwasababu hakuweza
kutembea katika Tunda la Roho Mtakatifu.
2Samweli 17;14
14 Naye Absalomu na watu wote wa
Israeli wakasema, Shauri la Hushai, Mwarki, ni jema kuliko shauri la
Ahithofeli. Kwa maana Bwana alikuwa amekusudia kulivunja shauri jema la
Ahithofeli, ili Bwana alete mabaya juu ya Absalomu.
2Samweli 17;23
23 Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa
shauri lake halikufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani
kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajisonga; akafa, akazikwa
kaburini mwa babaye.
Mstari wa 14-Absolumo aliomba
shauri la pili na Ahithofeli akatoa shauri ambalo kama lingefuatwa Daudi
angeangamizwa lakini Mungu alijibu ombi la Daudi hapo Daudi aliomba akiwa
anamkimbia Mwanawe Absalomu ‘’ Mtu mmoja akamwambia Daudi ya
kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee
Bwana, nakusihi, uligeuze shauri la Ahithofeli liwe ubatili.”(2Samweli
15;31). Daudi alijua karama ya Ahithofeli ndio maana alifanya ili ombi.
Shauri la Ahithofeli likakataliwa
sawasawa na Ombi la Daudi kwa Bwana,lilikuwa ni shauri jema kwa upande wa
Absolumo.
Nataka uone alichokifanya
Ahithofeli baada ya shauri lake jema kuachwa.Neno linasema alienda nyumbani
kwake akajitundika akafa.Karama kubwa lakini Tunda la Uvumilivu,Tunda la Upendo
halikuwa kwake,hakujua jinsi ya kustahimili kukataliwa,hakuwa na Tabia ndani
yake ambayo ingemvusha katika kipindi shauri lake limedharauliwa.Na sio kwamba
shauri lake lilikuwa Baya hapana bado lilikuwa ni jema,lakini lilipuuzwa
kwasababu nyuma kulikuwa na mkono wa Mungu.
Lakini huyu ndugu alisusa kwa
namna ya ajabu, alienda mbali aliona amedharauliwa sana akaamuwa
kujinyonga.Alipokosa uvumilivu mauti ikapata mlango wa kumwangamiza.Alisusa
akaijitenga na watumishi wenzake.
Je si hali kama hii tuliyonayo
ndani ya kanisa,ndani ya Wana wa Mungu.Watumishi kususa huduma,kujitenga kabisa
na Kanisa.Kondoo kurudi majumbani na kugoma kwenda katika kusanyiko kwa sababu
tu shauri lake lililojema halikusikilizwa.Kususa kazi ya Mungu kwingi
kunakolifanya kanisa lisitembee katika kiwango kile kilichokusuidiwa kwasababu
kina Ahithofeli wa Leo wamesusia Huduma kwasababu ya kudharauliwa na Karama zao
wameenda nazo nyumbani na taratibu mauti inawanyemelea katika utumishi wao.
Mwana wa Mungu Tunda la Roho
Mtakatifu ndio unachohitaji,Kususa ni tabia ya mwili.Angalia Wanandoa ambao ni
Wana wa Mungu kususiana ni kitu ya kawaida kwasababu shauri lake limekataliwa.
Karama haitakuvusha saa ya
kukataliwa,Karama haitakuvusha saa ya kudharauliwa bali Tabia ya Roho Mtakatifu
ndio itakuvusha.Sikwambii kuwa mwili hautaamka kukutaka ususe la hasha,lakini
ufishe kwa kuitikia Tunda la Roho Mtakatifu.
Unaacha kuimba unasema wapo
mwilini siwezi kuhudumu nao,unasusa unafikiri ndio upo Rohoni,ndugu yangu sasa
ndio unatembea mwilini haswa.
Haijalishi unaUimbaji wa kiwango
cha juu kiasi gani kama Huna Upendo na uvumilivu utaishia kususa tu huduma.
Wekeza kukua katika matunda ya
Roho Mtakatifu.
Naamini kuna kitu Yesu ameachilia
ndani yako na umepata hatua katika kujifunza kutembea katika Roho,kutembea
katika Matunda ya Roho Mtakatifu.
Mungu akitupaa Neema yake
tutaendelea wiki ijayo na somo hili.
Barikiwa sana mpendwa wa Bwana.
KUTEMBEA KATIKA ROHO-3
Reviewed by Unknown
on
8:31:00 PM
Rating:
No comments: