KUTEMBEA KATIKA ROHO
KUTEMBEA KATIKA ROHO.
Wagalatia 5:22-25
22 Lakini tunda la Roho ni upendo,
furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama
hayo hakuna sheria.
24 Na hao walio wa Kristo Yesu
wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende
kwa Roho.
BWANA YESU ASIFIWE mwana
wa Mungu.
Karibu tujifunze kwa pamoja
Neno la Mungu.Kama kichwa cha somo kinavyosema hapo juu,tutajifunza kwa Msaada
wa Roho Mtakatifu jinsi ya kutembea au kuenenda/kutembea katika
Roho.Tutaangalia mambo kadhaa wa kadhaa kwa kadiri Roho Mtakatifu
atakavyotuongoza.
Ni kawaida sana kusikia
mtu akisema hauko Rohoni au upo mwilini.Mpaka tutakapokuwa tumemaliza mfululizo
wa somo hili utakuwa umepata ufahamu mkubwa utakao kupa hatua kubwa sana katika
maisha yako ya kiroho.
Yohana 3
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni
mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7 Usistaajabu kwa kuwa
nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
Mtu anapookoka yaani
anapompokea Yesu Kristo,ndipo huwa anazaliwa mara ya pili.Kinachozaliwa upya ni
roho ya yule aliyeokoka.Baada ya kuokoa mtu anakuwa mpya kabisa katika roho yake,lakini
katika nafsi ile ile na mwili ule ule wa Zamani.
2Wakorinto 5;
17 Hata imekuwa, mtu akiwa
ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Upya huu unatokea katika
roho ya mtu,Roho Mtaktifu anamzaa mtu kwa upya.
Maana yake kuanzia hapo
anakuwa ni mtu mwenye roho mpya yaani kiumbe kipya ila katika mwili wa
zamani.Neno linasema miili yetu itabadilishwa katika Ufufuo hapo ndipo tutapata
miili mipya.Roho Mtakatifu ameuhisha roho zetu ila miili yetu bado
haijauhishwa.
Warumi 8
11 Lakini, ikiwa Roho yake
yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo
Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho
wake anayekaa ndani yenu.
23 Wala si hivyo tu; ila na
sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu,
tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.
Kwa maana hiyo baasi mtu
aliyeokoka ni mtu mpya katika mwili wa zamani,mwili wenye asili ya dhambi.Hii
ndio inayoleta jukumu sasa la mtu kuutisha mwili wake na matendo yake.Mtu
aliyeokoka anapaswa kuishi kwa kufuata roho yake akiongozwa na Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu anapomzaa
mtu upya huizaa roho yenye matunda yaliyotajwa hapo juu.Hivyo kama ataishi kwa
kufuata roho yake iliyozaliwa upya atatembea katika Matunda ya Roho Mtakatifu
yaliyomiminwa ndani ya roho yake alivyozaliwa mara ya pili.Matunda hayo ni haya
UPENDO,FURAHA,AMANI,UVUMILIVU,UTU WEMA,FADHILI,UAMINIFU,UPOLE na KIASI.
Haya ndio matunda ya Roho
Mtakatifu ambayo mwana wa Mungu anatakiwa kutembea katika hayo.Kuenenda katika
Roho ni kutembea katika matunda ya Roho mtakatifu,ni kutembea katika tabia za
Roho Mtakatifu.Kutembea katika Roho sio kutembea ukinena kwa lugha au ukiomba
kila mahali japo unaweza kuwa unafanya hivyo kwakuongozwa na Roho
Mtakatifu.Kutembea katika Roho ni kuishi kwa Upendo,ni kuishi kwa uvumilivu, ni
kuishi kwa uaminifu.Mtu yoyote anayetembea katika haya huyo ndiye mtu
anayetembea katika Roho.
Kutokana na kwamba mtu
aliyeokoka anaishi katika mwili ambao nao unamatunda yake,kunakuwa na upinzani
kwasababu mwili utataka kuutimiza matakwa yake,wakati huo huo roho ikitaka
kutimiza ya kwake.
Hivyo mtu anajukumu la
kuutiisha mwili,yaani kuufisha kabisa mwili ili usidhihirishe matunda
yake.Jukumu la kuufisha mwili ni la kwako wala si la Mungu.
Kuna vitu viwili ambavyo
ni matokeo ya Roho Mtakatifu kwenye maisha ya mtu.
1.Tunda la Roho Mtakatifu
(Wagalatia 5;22-23)
Hili mtu anapozaliwa mara
ya pili linakuwa ndani ya roho yake iliyozaliwa upya.
Kuanzia hapo anajukumu la
kukua katika matunda hayo kwa kufuata msukomo wa tabia hizi za Roho
Mtakatifu.Hizi kila aliyeokoka anazo na anapaswa kudhihirisha hizo tabia kwenye
maisha yake.Kama umeokoka unapaswa kudhihirisha tabia hizi kwasababu ni tabia
zilizoachiliwa ndani ya roho yako mpya siku ulipozaliwa.
2.Karama za Roho
Mtakatifu
Karama za Roho Mtakatifu
hizi huachiliwa na Roho Mtakatifu kwa mtu aliyeokoka kwa ajili ya kufanya kazi
kwenye ofisi ya Ufalme wa Mungu.Hizi ni zaidi ya Tabia,hivi ni vitendea kazi
kutokana na ofisi aliyopewa mtu katika zile ofisini tano alizotoa Yesu.
1Wakorinto 12;4-11.
4 Basi pana tofauti za karama;
bali Roho ni yeye yule.
5 Tena pana tofauti za huduma, na
Bwana ni yeye yule.
6 Kisha pana tofauti za kutenda
kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo
wa Roho kwa kufaidiana.
8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa
neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;
9 mwingine imani katika Roho yeye
yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;
10 na mwingine matendo ya miujiza;
na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na
mwingine tafsiri za lugha;
11 lakini kazi hizi zote huzitenda
Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.
Karama hizi huachiliwa
kutegemea kile ambacho Roho Mtakatifu amekusudia kukifanya kupitia Yule mtu kwa
wakati ule au kufuatana na Ofisi ya mtu katika mwili wa Kristo.
Waefeso 4:11-13
11 Naye alitoa wengine kuwa mitume,
na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji
na waalimu;
12 kwa kusudi la kuwakamilisha
watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;
13 hata na sisi sote tutakapoufikia
umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata
kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
Utaona Neno ili Huduma
itendeke,Yesu ndiye anayelijenga kanisa lake,ndiye anayekamilisha watakatifu
kupitia Ofisi hizi 5 alizotoa hapo.Kila ofisi inahitaji vitendea kazi yaani
karama ili huduma husika ifanyike.Karama hizi ndio hutolewa na Roho Mtakatifu
kulingana na ofisi na huduma inayokusudiwa kwa wakati ule.
Huwezi kuta Mwalimu anapewa karama
ya Unabii kwasababu ofisi yake hahiitaji Unabii kafanya huduma yake,lakini
Nabii hawezi kufanya huduma yake pasipo Karama ya Unabii.Japo inaweza kutokea
kutokana na huduma aliyokusudia Roho Mtaktifu kuifanya ndani ya kanisa akaachilia
Neema juu ya Mwalimu akahudumu kwa Roho ya Unabii kwa wakati huo na baada ya
kumaliza alichokusudia anabaki kuwa Mwalimu na vitendea kazi vingine
anavyovihitaji ili kuhudumia.
Mpaka hapo utaona tumejikuta tuna
karama za Roho Mtakatifu na Tabia au Tunda la Mtakatifu.
Kwa leo tuishie hapo mwana wa
Mungu,Tutaendelea week ijayo na sehemu ya pili.
Naamini Umepata Ufahamu mpya
ndani yako,usikose kufuatilia sehemu inayofuata ambako tutaingia ndani zaidi.
KUTEMBEA KATIKA ROHO
Reviewed by Unknown
on
7:30:00 PM
Rating:
No comments: