BREAKING NEWS

[5]

JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-I



    JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-I

Mithali 4;23  "Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima"

​​​​​ (Prov 4:23 [HCSB])

Guard your heart above all else, for it is the source of life.

(Prov 4:23 [ESV2011])

Keep your heart with all vigilance, for from it flow the springs of life.

Bwana Yesu asifiwe,karibu tujifunze kwa pamoja kwa Roho wa Kweli jinsi ya kulinda moyo wako.Somo letu litakuwa likitoka katika kitabu cha Mithali 4;23
Ni Neno ambalo linaweza likawa sio mara yako ya kwanza kulisikia lakini embu fungua moyo wako ili Mungu akufundishe kwa undani juu ya Mstari huu,nami naamini baada ya kusoma hutabiki na ufahamu uliokuwa nawo kabla ya kusoma na mfumo wa maisha wako utaathiriwa na ufahamu ambao neno hili litauachilia ndani yako.

Neno linasema Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo,maana huko ndiko zitokako chemichemi za Uzima"
Kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ni kuwa Unajukumu la kuulinda moyo wako,tena kuulinda kuliko yote ulindayo.
Tuanze kwaa kujifunza Moyo ni nini hasa hata tukatakiwa kuulinda kuliko vyote tunavyolinda.

Kwa lugha nyepesi Biblia inazungumzia Moyo kwa maana kama 4 hivi;
a)Moyo ni chanzo/kiini cha Uhai wa kitu.
b)Moyo ni kiungo cha mwili kinachosukuma damu
c)Moyo ni roho ya mtu na pengine biblia imezungumzia moyo kama nafsi ya mtu.

1Petro 3;4 inasema mtu yupo wa nje na yupo wa ndani (inner man the real you and the outer man)sasa moyo ambao hili neno linauongelea sio wa mtu wa nje ambao ni wa nyama bali ni moyo wa mtu wa ndani, lakini tunaweza kutumia moyo wa nyama kuelewa moyo tunaousemea,Moyo wa nyama ni reflection tu ya moyo wa mtu wa ndani,biblia za kiengereza zinzuzngumzia kama A spirit of Man,maana yake kama vile Moyo wa nyama ulivyo na umuhimu kwa hali ya mwili hivyo Moyo(spirit)ni muhimu kwa mtu wa ndani.Moyo wa nyama ndio unaohusika na kuhakikisha hali ya uhai ya mwili na kila kitu kinachohusika na mwili kukaa salama,moyo ukipata shida mwili wote unakuwa na shida.Kwa namna nyingine moyo ndio chanzo cha uhai wa mwili.

Andiko linalituongoza linatuambia kuwa sababu ya kuulinda moyo ni kwasasabu huko ndiko zitokako chemichemi za uzima.Kwa namna hiyo uangalie moyo kama jicho la chemechemi ambako ndani yake yanatoak maji yaitwayo uzima.Maana yake njia pekee ya kuhakikisha maji hayo yaliuzima yanaendelea kuwepo ni kuulinda hiyo chemichemi.

Ulinzi unaoweka kwenye kitu chochote hutegemea na Uthamani (Umuhimu) wa kitu chenyewe,ni wazi ulinzi alio nao Raisi sio sawa na ulinzi alionao mbunge,na kiwango cha Ulinzi huo kinaaamuliwa na Umuhimu wa kitu chenyewe,Rais ni kama mboni au Taa ya nchi,maana yake akipata shida yeye nchi nzima inapata shida,ukisoma (2Samweli 21;17)  Lakini Abishai, mwana wa Seruya, akamsaidia, akampiga Mfilisti, akamwua. Ndipo watu wa Daudi wakamwapia, wakasema, Wewe hutatoka tena pamoja nasi kwenda vitani, usije ukaizima taa ya Israeli.”

.Utaona Daudi alikoswa kuuwawa na Adui vitani,wanajeshi wake walimwambia Usitoke tena kuja vitani Usije ukaizima Taa ya Israel,hii inakuonyesha kuwa Daudi alikuwa ndio Taa ya nchi nzima na hivyo kumlinda yeye kulitakiwa kwa gharama yoyote ile hata kwa uhai wa wanajeshi wengine angelindwa na hata kama njia pekee ya kumlinda ilikuwa ni Kutokumleta vitani basi Israel walikuwa tayari kufanya hivyo.Na hii inatupa kuona kuwa kama Mungu anatutakaa tuulinde moyo kuliko vyote tuvilindavyo basi Moyo ni wa thamani kuliko vyote,Yesu aliwahi kuzungumzia Moyo kama Jicho la Mwili akisema kama Jicho likiwa safi yaani likiwa na Nuru basi mwili wote utakaa nuruni.Hivyo basi kitu pekee ambacho mwanadamu anatakiwa kuwekeza nguvu zake zote kukilinda ni moyo wake kwasababu uzima wake unategemea hapo,Naweza kusema Mungu aliposema linda moyo wako alimaanisha linda Uzima wako.

Ufanisi wa Kulinda kitu chochote unategemea kwa kiasi kikubwa Ufahamu aliona nao Mlinzi au mbinu za kiulinzi alizonazo Mlinzi.Jaribu kujuliza unalindaje kitu pasipo kujua kitu hicho kinalindwaje.Mungu aliposema Linda sana moyo wako,aliweka jukumu la Ulinzi wa moyo kwa mwenye moyo maana yake Wewe ni Mlinzi wa moyo wako na kama ni hivyo Kufanikiwa au kufeli kwako katika jukumu hili la kiulinzi linategemea sana Ufahamu uliona kuhusu Ulinzi wa moyo.Kwa kusema hivyo nataka tuingie sasa kwenye mzizi wa somo letu ili wewe Kama Mlinzi wa moyo wako ujifunze jinsi ya kuulinda moyo wako.

Kitu cha kwanza anachooshenyeshwa mlinzi anapopewa kazi ya kulinda kitu ni kuonyeshwa Malango.Kwasababu kama unalinda kitu ili kisiharibiwe lazima uweke nguvu kwenye maeneo ambayo yanaweza kumruhusu Mharibu (Adui) kukifikia hicho kitu.Kwa kusema hivyo nataka uelewe kuwa Moyo una milango ambayo kwa hiyo vitu huweza kuufikia,hivyo kuulinda moyo kunahusika sana na kuangalia hiyo milango.

Tuanzie kwenye maneno ya Yesu ndipo tutaelewa tunaulinda vipi moyo na tunaulinda na vitu gani hasa.

Mathayo 12;33-37

 Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana.Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa”

Yesu anazungumzia swala la kuufanya mti kuwa mzuri ili matunda yake yawe mazuri au kuufanya mti kuwa mbaya na matunda yake kuwa mabaya.Yesu alikuwa anazungumzia Moyo kwa lugha ya Mti,ambao utakapofanywa mbaya basi matunda yake yatakuwa mabaya na utakapokuwa mzuri moja kwa moja matunda yake yatakuwa mazuri,hapa matunda ya mti ambao ni moyo ni yale yote yanayotoka kwenye moyo wa mtu kwasababu matunda hutoka kwenye mti,na matunda ndiyo yanautambulisha mti au aslili ya mti kama ni mbaya au ni mzuri.Ndivyo ilivyo Maneno au matendo ya mtu ambayo ni matokeo ya mawazo yake yote hutegemea hali ya moyo,kumbuka tulisema moyo ni kama chemichemi itoayo maji,hivyo kama maji yanayotoka ni maji machungu au matamu ni swala la aina ya mwamba inakoanzia chemichemi.Kama jicho la chemichemi lisivyo na sehemu ya kuamua aina ya maji yanayotiririka juu yake vivyo hivyo Kinywa cha mtu hakina sehemu katika kuamua aina ya maneno ambayo mtu anayasema.Yesu aliwashangaa sana kwa Kuwaambia enyi uzao wa nyoka mwawezaje kunena mema mkiwa wabaya,halafu anaendelea mbele kusema kwa maana kichwa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake,kilichomshangaza Yesu ni kwasababu yeye alikuwa anaijua principle ya Mti kutoa matunda yafananayo na asili yake,kinyume na hawa ambao Yesu akiijua mioyo yao yaaani asili ya mti ni mbaya lakini wakawa kwa vinywa vyao wanaongea mema.Naweza kusema kwa maneno(matunda)yako hali ya moyo wako itajulikana,Mithali inasema ingawa chuki yaweza kufichwa moyoni,itadhihirika tu mbele za kusanyiko,mtu anaweza kuwa na chuki lakini kwa kufunga kinywa chake ataificha na kuiweka akiba,na akiba hiyo huwekwa kwenye,moyo na anaweza kuongea maneno mazuri lakini hayana ukweli wowote nayo ni unafiki kwasababu mtu mwema katika akiba njema ya moyo wake hutoa mema na mtu mbaya katika akaba ya moyo wake hutoa uovu.Na chuki hiyo endapo haitaondolewa itadhihirika tu iwe ni kwa kinywa au kwa matendo.

Mithali 26;24-26..Achukiaye huficha chuki kwa midomo yake; Naye huweka akiba ya hila moyoni mwake.Anenapo maneno mazuri usimsadiki; Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake. Ingawa chuki hufunikizwa Kwa hila; Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko.


Marko 7;18-23 Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni. Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote. Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.KWA MAANA NDANI YA MIOYO YA WATU HUTOKA MAWAZO MABAYA, UASHERATI,WIVI, UUAJI, UZINZI, TAMAA MBAYA, UKOROFI, HILA, UFISADI, KIJICHO, MATUKANO, KIBURI, UPUMBAVU.HAYA YOTE YALIYO MAOVU YATOKA NDANI, NAYO YAMTIA MTU UNAJISI.

Maneno haya aliyasema Yesu lilipokuwa limetokaea swala la Utata wa kunawa mikono kabla ya kula huku Mafarisayo wakisema alaye pasipo kunawa mikono atatiwa unajisi maana mikono yake ni najisi na hivyo atakinajisi chakula,lakini kwa majibu ya Yesu anatuonyesha kuwa kinachomtia mtu unajisi ni kile tu kinachotoka kwenye Moyo wake,na hivyo chakula ambacho mtu anapokula hakiendi moyoni bali tumboni kisha kwenda chooni hicho hakiwezi kumtia mtu unajisi.Yesu anasisitiza tena Kuwa ndani ya moyo ndiko yanakotoka maovu yanayomtia mtu unajisi na chakula kingiweza tu kumtia mtu unajisi kama kingekuwa kinaweza kuingia kwenye moyo na kuathiri hali ya moyo.


Swali la Msingi la kujiuliza hapa ni huu uovu anaosema Yesu kuwa unatoka ndani ya moyo,Huwa unafikaje hapo kwenye moyo,Kumbuka hapo juu amesema mtu mwema kutoka kwenye akiba ya moyo wake,,maana yake huo Uovu ni akiba na kama ni akiba basi iliwekwa.
Kama vile mtu anapokula chakula huingia tumboni na kuwekwa akiba tumboni,vivyo hivyo mtu anapokula chakula kinachoweza kuingia moyoni hicho huwekwa akiba moyoni.

Maana yake ni hii chakula chochote kinachoweza kuingia kwenye moyo hicho kinaweza kuamua moyo uwe na akiba njema au mbaya.Kama vile mtu wa nje alivyo na mdomo wa kula hivyo hivyo mtu wa ndani ana mdomo wa kula chakula ambacho huingia ndani ya moyo na kuwa kuhifadhiwa kama akiba.Sicho kiingiacho kwa mdomo wa mwili kimtiacho mtu unajisi bali kiingiacho kwa Mdomo wa Moyo.

Naamini umepata Kitu.Kwa Neema ya Mungu tutaendelee na sehemu ya pili ya Somo hili.
Tutaendelea kwa Kuangalia Vinywa vya Moyo.Usikose mwendelezo wake.

Neema na Amani zitokazo kwa Bwana Yesu ziongezwe kwako kwa Kumjua Kristo.
JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-I  JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-I Reviewed by Unknown on 12:30:00 PM Rating: 5

14 comments:

Sora Templates