JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-3
JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-3
Neno la Kusimamia.
Mithali 4;23 "Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima”
Karibu tuendelee kujifunza jinsi ya Kulinda Moyo,leo tutamalizia
somo letu hili.
Tatazame maandiko kidogo kuhusu macho yako.
Kama tulivyokwisha kuona hapo juu kuwa macho yako ni kinywa cha
moyo wako, ukilitambua hili Hutakuwa mpumbafu na kula kila kitu.Huwezi
ukaanglia kila kitu kwasababu unapoangalia wewe unafikiri unaangalia lakini ukweli
ni kwamba moyo wako unakuwa unakula.
,Habakuki 1;13. Wewe
uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu,
Maneno ya Habakuki akizitaja sifa za Bwana Mtakatifu wa Israel, anazungumza
juu ya Mungu kuwa na Macho matakatifu kiasi ambacho hawezi kuutazama Uovu. Mungu
ni mtakatifu sana na Utakatifu huo ndio Habakuki anausemea kama Usafi wa macho
ambao kwa jinsi ulivyo mkuu sana macho yake hayawezi kutazama Uovu,Neno la
Mungu linasema Mungu anakaa ndani yetu na Zaidi Mungu alisema Nanyi mtakuwa
Watakatifu kwa kuwa mimi ni Mtakatifu,sasa jaribu kufikiri huyu Mungu
aliyemtakatifu asiyeweza kutazama Uovu anaishi ndani ya Moyo wako,na amesema
wewe wapaswa kuwa Mtakatifu kama yeye,Utakatifu huo ndio uliomfanya asiweze
kutazama Uovu.Mtu aliyeokoka hawezi kutazama kila kitu maana Mungu aliyendani
yake hawezi kutazama kila kitu.
Kwasababu ya kukosa Ufahamu huu wana wengi wa Mungu wameeangamia na
hata sasa wanaangamia na cha ajabu ni kuwa hata wengine wanatetea juu ya
vyakula wanavyokula(Vitu wanavyovisikiliza na wanavyovitazama).Kinachosikitisha
na kushangaza ni kuona jinsi watu wanavyokuwa waangalifu juu ya aina ya vyakula
na vinywaji wanavyomlisha mtu wa nje,utasikia mtu akikwambia nina aleji na
Maharage,ooohh soda nyeusi ni mbaya kwa afya yangu,wapo watu wasiokula baadhi
ya vyakula kwasababu tu kwao vinaonekana vyakula rahisi yaani vyakula vya
kimaskini kwa lugh ya wazungu utawasikia wakisema “This food is too cheap,this
kind of food is not my type” wao kul ugali kwao ni kujishusha
thamani.Watazame Waimbaji wanavyochagua vyakula na vinywaji na juhudi hizi zote
ni kwa ajili ya mtu wa nje ambaye ni mavumbi asiye wa kudumu.Lakini mtu wa
ndani(moyo) ambaye ni wa kudumu huyo hapewi thamani,huyo anaonekana anastahili
kula kila kitu hata kama ni sumu huyo wanamlisha tu wasichokijua ni kwamba ni
bora Sumu anayokula mtu wa nje ambaye anaweza tu kupewa mziwa kwa dakika chache
sumu ikatoka akawa mzima au kwa kuwekewa drip ya maji na damu yake ikawa
safi,tofauti na sumu anapopewa ntu wa ndani ni hatari sana,gharama ya kuiondoa
hiyo sumu na madhara yake ni kubwa sana na inaweza kuchukua miaka kuindoa hiyo
sumu kwenye moyo wa mtu.Watu waliowahi kula sumu ya picha za uchi
“phonograph” (ndio nasema Sumu ili kila
alaye ajue anajiua mwenyewe)na sasa wameokoka wanaweza kushuhudia vizuri
gharama waliyolipa na pengine bado hata sasa wanalipa kwa kupitia Utakaso wa
Neno la Mungu ambalo ni Maziwa yasiyoghushiwa ili kuitakasa mioyo yao na
kuiondoa hiyo sumu ndani ya mioyo yao.
Waefeso 5;25-27.
“Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda
Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji
katika neno;apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo
lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa”
Neno hili limekuja kwa lengo la kukupa ufahamu utaobadilisha mfumo
wa maisha yako ambao huo umekuwa ukiharibu moyo wako na matokeo yake badala ya
moyo kububujika maneno yenye munyu na mawazo mema unabubujika matusi,mawazo ya
tamaa na uzinzi.
Moyo wako ni wa thamani sana Uhai wako unategemea hali ya huyo mtu
wa ndani,kama vile unavyoweza kusema This kind of food is not my type kwa ajili
ya mwili vivyo hivyo mtu wa ndani ni wa thamani sana,,,not every kind of food
is worth feeding him,,remember only a fool feeds on trash.Acha kula jalalani.Be
selective acha kuangalia miziki ya kidunia inayoutukuza Uzinzi na kuwasha moto
wa tamaa ndani yako.Acha kuwa na kiburi kwa kusema kwani kusikiliza huo muziki
kunashida gani,husikilizi unakula.
Acha kunywa sumu ya phonograph maana hakika utakufa, Ni sumu ya
hatari sana ni sawa na wadudu wanaokula mizizi ya mti baada ya muda mti
utaanguka pasipo watu kujua.Ni dhambi inayoshambulia maisha yako ya sirini, huko
ambako ndiko ulipaswa kukitaa mizizi ya maisha ya Utakatifu.
Vijana wengi walio ndani ya kanisa na walio nje wapo kwenye gereza
hili. Na ubaya wa gereza hili ni kwamba ni gereza la Sirini.Pasipo mfungwa
mwenyewe kuamua kutafuta msaada hakuna mtu anayeweza kujua kuwa mpendwa yupo
gerezani.
Kama tayari upo kwenye gereza la picha hizi za Uchi zinzojazaa
Uchafu kwenye moyo wako, tafuta msaada wa Yesu Kristo ili utoke hapo.
Kwasababu sio vita unayoweza kutoka mwenyewe pasipo msaada wa
Mungu.
Tafuta Mtumshi wa Mungu aliyehai ambaye ndani yako unasikia amani
kusema naye,ili kwa pamoja mvipige vita hivyo ili utoke hapo.Uwe huru kwa maana
ni hakika kila atazamaye Uchafu huu ni mtumwa wa Ibilisi.Nyuma ya hizo picha
ipo roho iliyokufunga ndio maana jitihada zako za kuacha zinafeli kila siku.Ni
mpaka Roho yenye nguvu (Roho ya Yesu) kuliko hiyo roho iingilie kati ndio
unaweza kutoka kwenye gereza hilo la picha za ngono linaloharibu moyo wako.
Yohana 8:34
Yesu akawajibu, Amin, amin,
nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
2Peter 2:19
wakiwaahidia
uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa
mtumwa wa mtu yule.
Acha kuambatana na marifiki ambao stori zao ni kuhusu uzinzi, uchafu
na tamaa.
Linda moyo wako linda uzima wako, kama ulishaharibika Urudishe kwa
aliyeufinyanga aufinyange upya, kwa Roho Mtakatifu kwa maji katika Neno lake.
Neema ya Yesu Kristo iwe juu yako kukuwezesha kuliishi neno hili
na hatimaye kufanikiwa kuulinda moyo wako ili Uzima uzidi kububujika kinywani
mwako kutoka kwenye moyo wako.
JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-3
Reviewed by Unknown
on
5:43:00 PM
Rating:
Somo zuri barikiwa
ReplyDeleteSomo zuri sana hili nimebarikiwa sana
ReplyDelete