BREAKING NEWS

[5]

MJUE MUNGU ILI UWE NA AMANI-1



MJUE MUNGU ILI UWE NA AMANI-1

 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.

Ayubu 22;21


Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu.
Nasikia ndani yangu kusema na wewe juu ya KUMJUA MUNGU.

Neno hapo juu linaweka wazi kuwa Kuwa na Amani kunategemea na vile mtu anavyomjua Mungu.
Amani inayozungumziwa hapa ni amani ya ndani ya moyo,ni ILE SALAMA YA ROHONI.
Ni ile AMANI INAYOUTAWALA MOYO si katika nyakati za furaha na mambo yanaenda,bali ni AMANI inayotawala moyo wa mtu hata katikati ya dhiki na dhoruba.

Niongee Neno gumu kidogo,Amani ya Yesu ni Amani ambayo kutawala kwake hakutegemei hali ya ushwari wa bahari,la hasha ni AMANI ambayo inatawala katika vipindi vyote vya maisha.Na kama mwana wa Mungu wewe unasubiri hali ya bahari itulie ndipo Uwe na Amani ya Yesu,nikwambie wazi unaweza ukasubiri sana miaka mingi.Kwasababu kwenye maisha kila siku kuna Uovu unaotosha kukuvurugia amani yako kama Humjui Mungu.Sasa haya ni maneno ya Yesu mwenyewe aliposema katika Mathayo 6; 34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

Maneno haya -yatosha kwa siku maovu yake ni Kweli ya Yesu kuwa kwenye kila siku yapo masumbufu yanayoweza kumnyima mtu amani.Lakini Yesu anatutaka tuwe na Amani saa zote,na Ametupa Amani yake inayotawala katika siku zote,Amani ya Yesu haitegemei kabisa hali ya mazingira ya nje,bali Ufahamu wa mtu juu ya Mungu,nikufikirishe tu kidogo,kama Amani ya Yesu ingekuwa inategemea ushwari wa hali ya bahari unafikiri katika maisha haya yenye mawimbi ya kila siku,nani angeifaidi Amani ya Yesu.?Lakini amani yake haitegemei kabisa hali ya nje,bali vile unavyomjua Mungu.Angalia jambo hili.Yesu alikuwa pamoja na wanafunzi bahari kwenye boti.
Yeye amelala zake kwa starehe,Wanafunzi wanataabika na kuhangaika.Kama unajua kuwa Kulala kunategemea amani ya ndani unaweza kuelewa kuwa Yesu alikuwa na amani ndani yake wakati bahari imechafuka mawimbi.Wanafunzi wanataharuki yeye amelala.Na kinachofurahisha ni swali walilomuuliza walippoenda kumwamsha,Mwalimu si kitu kwako kuwa tunaangamia?
Katika hili swali utaona wanafunzi kiliwasumbua sana,yaani wakati wao wanaona Kuangamia kwasababu ya tufani,Yesu wala hana mpango,yeye yupo zake kalala,Waliona kana kwamba hajali kabisa hali ya bahari?

Lakini jibu la Yesu lilionyesha kilichomfanya yeye alale kwa starehe,aliwauliza Hamna Imani bado?.
Sasa Imani inazalishwa na Ufahamu wako juu ya Mungu,na Imani huzalisha amani ndani ya moyo.
Kilichowatofautisha hapa ni jinsi walivyomjua Mungu,Yesu alimjua Baba yake,hivyo akawa na amani inayompa hata usingizi kwenye tufani.Hiyo ndio amani ya Yesu.Yaangalie maisha yako sasa hivi,anagalia mawimbi ya bahari,halafu angali ndani yako je Una amani,Je unaweza kulala kama Yesu alivyokuwa amelala wakati bahari imechafuka?
Au nawewe unamuuliza Mungu hivi kweli Unajali maisha yangu?
Hivi Yesu unawezaje kutulia katika hali ninayopitia,Je Bwana Yesu huoni kuwa naangamia?
Marko 4;35-40

 35 Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo.

 36 Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.

 37 Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.

 38 Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?

 39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.

 40 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?

Dhoruba ilitosha kumnyima Yesu amani na kumfanya asilale,lakini kwasababu Yesu alimjua Baba yake,haikuwa hivyo kwake.
Yesu anataka uwe na amani na uweze kalala katikati ya tufani inayoendelea kwenye boti ya maisha yako.

Mungu akubariki na kukupa amani.Tutaendelea kwa kadiri Mungu atakavyotupa Neema yake.
MJUE MUNGU ILI UWE NA AMANI-1 MJUE MUNGU ILI UWE NA AMANI-1 Reviewed by Unknown on 10:05:00 AM Rating: 5

11 comments:

  1. Amina mtumishi wa Mungu nimebarikiwa na somo

    ReplyDelete
  2. Harrah's casino to go public - Aljordan14 retromegabit
    Harrah's air jordan 18 retro racer blue to you will not run jordan 18 white royal blue to my site a air jordan 18 stockx shop casino in air jordan 18 retro yellow suede from me the Ak-Chin area. The show air jordan 18 retro men red casino will have a gaming floor at Harrah's in Ak-Chin Village.

    ReplyDelete
  3. Barikiwa sana na Bwana ndugu kwa mafundisho mazuri

    ReplyDelete
  4. Mungu akubariki mtumish wa mungu

    ReplyDelete
  5. Ubarikiwe mtumishi was Bwana

    ReplyDelete
  6. Nimebarikiwa sana

    ReplyDelete
  7. Mungu akubariki sana mtumishi

    ReplyDelete
  8. Asante kwa fundisho zuri. Mungu akubariki

    ReplyDelete

Sora Templates