MJUE MUNGU ILI UWE NA AMANI-1
MJUE
MUNGU ILI UWE NA AMANI-1
Ayubu
22;21
Bwana
Yesu asifiwe mwana wa Mungu.
Nasikia
ndani yangu kusema na wewe juu ya KUMJUA MUNGU.
Neno
hapo juu linaweka wazi kuwa Kuwa na Amani kunategemea na vile mtu anavyomjua
Mungu.
Amani
inayozungumziwa hapa ni amani ya ndani ya moyo,ni ILE SALAMA YA ROHONI.
Ni
ile AMANI INAYOUTAWALA MOYO si katika nyakati za furaha na mambo yanaenda,bali
ni AMANI inayotawala moyo wa mtu hata katikati ya dhiki na dhoruba.
Niongee
Neno gumu kidogo,Amani ya Yesu ni Amani ambayo kutawala kwake hakutegemei hali
ya ushwari wa bahari,la hasha ni AMANI ambayo inatawala katika vipindi vyote
vya maisha.Na kama mwana wa Mungu wewe unasubiri hali ya bahari itulie ndipo
Uwe na Amani ya Yesu,nikwambie wazi unaweza ukasubiri sana miaka
mingi.Kwasababu kwenye maisha kila siku kuna Uovu unaotosha kukuvurugia amani
yako kama Humjui Mungu.Sasa haya ni maneno ya Yesu mwenyewe aliposema katika
Mathayo 6; 34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Maneno haya -yatosha kwa siku maovu yake ni Kweli ya Yesu kuwa kwenye
kila siku yapo masumbufu yanayoweza kumnyima mtu amani.Lakini Yesu anatutaka
tuwe na Amani saa zote,na Ametupa Amani yake inayotawala katika siku zote,Amani
ya Yesu haitegemei kabisa hali ya mazingira ya nje,bali Ufahamu wa mtu juu ya
Mungu,nikufikirishe tu kidogo,kama Amani ya Yesu ingekuwa inategemea ushwari wa
hali ya bahari unafikiri katika maisha haya yenye mawimbi ya kila siku,nani
angeifaidi Amani ya Yesu.?Lakini amani yake haitegemei kabisa hali ya nje,bali
vile unavyomjua Mungu.Angalia jambo hili.Yesu alikuwa pamoja na wanafunzi
bahari kwenye boti.
Yeye amelala zake kwa starehe,Wanafunzi wanataabika na kuhangaika.Kama
unajua kuwa Kulala kunategemea amani ya ndani unaweza kuelewa kuwa Yesu alikuwa
na amani ndani yake wakati bahari imechafuka mawimbi.Wanafunzi wanataharuki
yeye amelala.Na kinachofurahisha ni swali walilomuuliza walippoenda
kumwamsha,Mwalimu si kitu kwako kuwa tunaangamia?
Katika hili swali utaona wanafunzi kiliwasumbua sana,yaani wakati wao
wanaona Kuangamia kwasababu ya tufani,Yesu wala hana mpango,yeye yupo zake
kalala,Waliona kana kwamba hajali kabisa hali ya bahari?
Lakini jibu la Yesu lilionyesha kilichomfanya yeye alale kwa
starehe,aliwauliza Hamna Imani bado?.
Sasa Imani inazalishwa na Ufahamu wako juu ya Mungu,na Imani huzalisha
amani ndani ya moyo.
Kilichowatofautisha hapa ni jinsi walivyomjua Mungu,Yesu alimjua Baba
yake,hivyo akawa na amani inayompa hata usingizi kwenye tufani.Hiyo ndio amani
ya Yesu.Yaangalie maisha yako sasa hivi,anagalia mawimbi ya bahari,halafu
angali ndani yako je Una amani,Je unaweza kulala kama Yesu alivyokuwa amelala
wakati bahari imechafuka?
Au nawewe unamuuliza Mungu hivi kweli Unajali maisha yangu?
Hivi Yesu unawezaje kutulia katika hali ninayopitia,Je Bwana Yesu huoni
kuwa naangamia?
Marko 4;35-40
35 Siku ile kulipokuwa
jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo.
36 Wakauacha mkutano,
wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja
naye.
37 Ikatokea dhoruba kuu ya
upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.
38 Naye mwenyewe alikuwapo
katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu
kwako kuwa tunaangamia?
39 Akaamka, akaukemea
upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.
40 Akawaambia, Mbona
mmekuwa waoga? Hamna imani bado?
Dhoruba
ilitosha kumnyima Yesu amani na kumfanya asilale,lakini kwasababu Yesu alimjua
Baba yake,haikuwa hivyo kwake.
Yesu
anataka uwe na amani na uweze kalala katikati ya tufani inayoendelea kwenye
boti ya maisha yako.
Mungu akubariki na kukupa amani.Tutaendelea kwa kadiri Mungu atakavyotupa Neema yake.
MJUE MUNGU ILI UWE NA AMANI-1
Reviewed by Unknown
on
10:05:00 AM
Rating:

Amina mtumishi wa Mungu nimebarikiwa na somo
ReplyDeleteAmina asante sana kwa neno hili
ReplyDeleteHarrah's casino to go public - Aljordan14 retromegabit
ReplyDeleteHarrah's air jordan 18 retro racer blue to you will not run jordan 18 white royal blue to my site a air jordan 18 stockx shop casino in air jordan 18 retro yellow suede from me the Ak-Chin area. The show air jordan 18 retro men red casino will have a gaming floor at Harrah's in Ak-Chin Village.
Barikiwa sana na Bwana ndugu kwa mafundisho mazuri
ReplyDeleteMungu akubariki mtumish wa mungu
ReplyDeleteUbarikiwe mtumishi was Bwana
ReplyDeleteNimebarikiwa sana
ReplyDeleteMungu akubariki sana mtumishi
ReplyDeleteGod bless u
ReplyDeleteAsante kwa fundisho zuri. Mungu akubariki
ReplyDeleteAsante kwa somo
ReplyDelete