BREAKING NEWS

[5]

NEEMA YA MUNGU INAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUSHINDA MAJARIBU NA KUISHI MAISHA YA USHINDI KATIKA ULIMWENGU HUU-3



 NEEMA YA MUNGU INAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUSHINDA MAJARIBU NA KUISHI MAISHA YA USHINDI KATIKA ULIMWENGU HUU-3



Kuelewa kuhusu Neema
Baada ya kuangalia na kulewa aina na mazingira ya ulimengu tunaoishi na kabla ya kuelewa namna ambavyo neema inaweza kukusaidia ni muhimu kuelewa kuhusu neema yenyewe sasa ni wakati sahihi kuelewa maana ya neema ya Mungu. Na katika kuelewa hili ni vizuri kuona maandiko yanasemaje.

Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni. Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.” Warumi 4:4-5

Katika maneno hayo tunaona kuwa neema ni kupewa usichostahiri kupewa, Kama kuna kitu umekifanyia kazi, ujira wake sio neema kwako bali ni stahiri yako. Lakini kama hujafanyia kazi hakuna unachostahiri, lakini ukipewa usichostahiri, kinahesabiwa kuwa neema. Kwa kuwa anayetakiwa kupewa ni yule aliyestahiri au yule ambaye ni haki yake, kwa hiyo neema inakutengezea mazingira au inakuweka mahali pa kustahiri kupokea usichostahiri kupokea.

Kumbuka Mungu ni mwenye haki, kwa hiyo humpa kila mtu anachostahiri. Kuna wakati tunakuwa mahali ambapo hatuwezi kufikia vitu vingine, kwa hiyo anatumia neema kukuleta mahali pa kustari ili kuweza kupokea. Mfano, mwanadamu alipoasi, alistahiri adhabu na akaingia kwenye utumwa, kwa sababu hiyo alihitaji ukombozi. Nafasi yake ilikuwa haipi kustahiri ukombozi huo. Ingawa Mungu aliweka tayari ukombozi huo, lakini mwanadamu hakuwa kwenye nafasi ya kuupokea. Kwa hiyo Mungu anampa mtu neema kumleta mahali pa kustahiri kupokea wokovu. Neema humpa mtu nafasi ya kuufikia wokovu.

Kwa manane mengine tunaweza kusema, neema ni fursa ya kulifikia jambo usiloweza kulifikia. Kila ambacho huwezi kukifikia kwa kiinadamu, neema itakufikisha pale. Pale ambapo matendo yako hayawezi kukufikisha, neema itakufikisha hapo.

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;” Waefeso 2:8

Mstari unatusaidia kuelewa zaidi kuhusu neema. Kitu kisichotokana na nafsi zetu, juhudi zetu, lakini tumepewa, kilichofanya tupokee ni neema. Na hiyo neema ni kipawa cha Mungu. Kipawa hufanyii kazi kukipata bali hupewa bure. Inategemea huruma za yule anayekupa.

KUJIFUNUA AU KUDHIHILIKA KWA NEEMA

Imekuwa changamoto kubwa pale ambapo Mungu anaachilia neema yake kwa mtu lakini huyo mtu anakuwa hajui kuwa neema ya Mungu imeachiliwa juu yake. Hii ni kwa sababu kinachooneka kwa macho ni matokea ya kutenda kazi kwa neema kuliko neema yenyewe. Watu wanapoona mambo yanavyotokea wanashindwa kuelewa kuna kutenda kazi kwa neema nyuma yake. Mara zote, unachokipokea sio neema bali kilichofanya hayo upokee ni neema. Kilichotokea nyuma ya pazia ndio neema, ambayo inafanya kazi ya kufunua kitokee nje. Hutumika neema kuvipokea vitu vya Mungu, kwa hiyo neema ndiyo inayotupa nafasi kuvifikia vitu vya kimungu.

Neema hujifunua kwa namna mbalimbali, la muhimu kujifunza ni kujua pale neema inapojifunua. Kutokana na namna tofauti ambavyo neema hujifunua, tunaweza kuangalia kwa jumla namna inavyojifunua.

a. Kupitia wema wake

ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.” Waefeso 2:7

Biblia inasema, Mungu audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi, na atafanya hivyo kwa njia ya wema wake. Neema ya Mungu hujfunua kupia wema wa Mungu katika maisha ya mtu. Tunapoona wema wa Mungu maishani mwetu, tunajua kwa hakika ni kujifunua kwa neema. Mungu ni mwema kwa wenye dhambi na wasio na dhambi, anapowapo wema wake, sio kwamba wanastahiri lakini kwa sababu ya kutenda kazi kwa neema yake. Anapowanyea mvua wenye haki na waovu, ni udhirisho wa neema yake katika maisha ya hao watu.

Kujifunua kwa neema kwa njia ya wema wa Mungu, ni pana sana kwa maana kwamba wema wa Mungu, inahusisha karibia matendo yote ya Mungu anayoyafanya katika maisha yetu. Unapoona wema wa Mungu unajifunua kwako, ujue Mungu anafunua wingi wa neema. mfano, upo kwenye mazingira ya kwamba unatakiwa kulipia malipo fulani muhimu na leo ndio siku ya mwisho kulipia, alafu unamwomba Mungu akufungulie mlango wa kupata pesa lakini mpaka jioni inafika hujapata pesa na bado hujui unapataje. lakini kesho inafika usikia mwisho wa kulipia umeongezwa mpaka baada ya siku mbili na kumbe siku hiyo ndiyo unapokea mshara wako unalipia malipo yako. Hiyo ni neema, katika wema wa Mungu ilikuwa katika Muda. Muda ndio uliobeba neema.

b. Kupitia ufahamu na maarifa

Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;” Tito 2:11-12

Neema ya Mungu ili ikuooe ni lazima ifunuliwe, isipofunuliwa inakuwa haina nguvu juu yako. Mungu ni Mungu wa neema, na alikuwa na neema tangu mwanzo, lakini haikuweza kutuokoa mpaka ulipofika wakati timilifu, alipoifunua hiyo neema kwetu na sasa tunaokolewa kwa hiyo neema. Na hiyo neema hujifunua kwa kuachilia ufahamu na maarifa ndani yatu juu ya kile ambacho Mungu anataka kukuokoa. Ona neno hili, “…..nayo yatufundisha……’ Sio tu neema, bali neema iliyofunuliwa. Neema ikifunuliwa juu yako, inaachila mwangaza juu ya namna ya kufanya na kushughurikia jambo fulani.

Mungu akaitaka kukusaidia juu ya jambo fulani, anaachilia neema yake itakayokupa ufahamu namna ya kushughurikia jambo hilo. Mfano, Biblia inasema “iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti” (Mithali 14:12) Kuna njia unaweza ukawa umechukua na usijuae kuwa umekosea kabisa. Katika kukusaidia, Mungu anaachilia na kufunua neema yake kwako ambayo itakupa ufahamu juu ya mahali ulipo na unakotakiwa kwenda. Gafla ndani yako unapata ufahamu ndani yako kuwa jambo unalolifanya sio sahihi. Baada ya hapo kazi inakuwa kwako, kurudi ama kuendelea hivyo hivyo.

Mungu anapokupa maarifa na ufahamu juu ya ufalme ujue neema yake imefunuliwa kwako, ili uweze kwenda sawa na huo ufahamu. Kuna wakati ambao Mungu huachilia neema yake, na kukupa nafasi ya kufikia sehemu fulani ya maarifa, ikiwa na maana anakuhitaji mahali kwa utumishi. Ile neema inakuwa dhahiri kwako na kujua wapi unakoelekea. Nafasi ya kupata maarifa na ufahamu fulani inakuja kwa sababu ya neema iliyofunuliwa ndani yako, na hii inakuwa ishara kuwa Mungu anakupeleka mahali fulani. Mungu anakupa nafasi ya kujiendeleza kielimu na kuongeza maarifa, hiyo nafasi huja kwa neema inayoachiliwa kwako kwa sababu iko nafasi inayokusubiri.

Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.” Mithali 3:3-4
Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako, Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako.” Mithali 1:8-9

Kwa maneno mengine mithali inatuambia fursa ya kupata mafundisho na kusikia sheria ni udhihirisho wa neema, Mafundisho hayo na sheria yanatengeza nafasi ya kushughurikia ipasavya mambo yaliyoko mbele yako. Njia pekee ya ushughurikia jambo linapokuwa ni kupata ufahamu na maarifa, neema ya Mungu kufunuliwa kufungua njia hiyo kwa kukupa maarifa na ufahamu ili uweze kushughurikia hilo swala.

 c. kupitia mambo/matendo yanayofanyika

Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao, watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana. Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba, aende hata Antiokia. Naye, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.” Matendo 11:21-23

Jambo la muhimu kujua ni kuwa neema huonekana. Baada ya Barnaba kufika Antiokia, alifanikiwa kuona neema ya Mungu kwa watu, akafurahi. Barnaba alifanikiwa kuiona neema hiyo ya Mungu kwa kuangalia mambo au matenda ambayo yalikuwa yanafanyika huko Antiokia. Biblia inasema, mkono wa Bwana ukawa pamoja na mitume, wengi wakamwelekea Bwana kwa kumwamini. Alipoyaona matendo yaliyokuwa yakiendelea kufanyika, akaona neema. Ikiwa na maana kuwa yale matendo yalikuwa yanafunua neema ya Mungu kiasi ambacho anaweza akaona hiyo neema katika matendo. Kupitia matendo yanayofanyika una uwezo wa kuona neema iliyo juu ya mtu, watu, eneo au juu yako.

Mfano, ingawa neema ya Mungu ilikuwa haitajwi mara kwa mara katika agano la kale lakini matendo amboyo Mungu alikuwa anafanya, yalikuwa ni matendo ya neema. Kwa kuangalia jinsi Mungu alipokuwa akibakisha mabaki ya watu wakati walistahiri kuangamizwa taifa lote. Kupitia hii unaona neema ambayo Mungu alikuwa anaachilia kwa taifa.

Kwa mfano, biblia inasema hivi:-

Bwana asema hivi, Watu wale walioachwa na upanga walipata neema jangwani; yaani, Israeli, hapo nilipokwenda kumstarehesha.” Yeremia 31:2

Ingawa Mungu alitaka kuwaangamiza wote, lakini neema yake ilifanya asiangamize wote bali abakishe mabaki. Hayo mabaki yaliyosalia yalitokana na neema iliyoachiliwa juu ya taifa ili kuwaokoa lasivyo taifa lote lingefutiliwa mbali.

Itaendelea, fuatilia mfululizo huu

Itaendelea, fuatilia muendelezo

NEEMA YA MUNGU INAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUSHINDA MAJARIBU NA KUISHI MAISHA YA USHINDI KATIKA ULIMWENGU HUU-3 NEEMA YA MUNGU INAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUSHINDA MAJARIBU NA KUISHI MAISHA YA USHINDI KATIKA ULIMWENGU HUU-3 Reviewed by Unknown on 2:18:00 PM Rating: 5

3 comments:

Sora Templates