NEEMA YA MUNGU INAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUSHINDA MAJARIBU NA KUISHI MAISHA YA USHINDI KATIKA ULIMWENGU HUU-3
NEEMA YA MUNGU INAVYOWEZA
KUKUSAIDIA KUSHINDA MAJARIBU NA KUISHI MAISHA YA USHINDI KATIKA ULIMWENGU HUU-3
Kuelewa
kuhusu Neema
Baada ya kuangalia na kulewa aina na mazingira ya ulimengu tunaoishi na kabla
ya kuelewa namna ambavyo neema inaweza kukusaidia ni muhimu kuelewa kuhusu
neema yenyewe sasa ni wakati sahihi kuelewa maana ya neema ya Mungu. Na katika kuelewa hili ni vizuri kuona maandiko yanasemaje.
“Lakini kwa mtu
afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni. Lakini
kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa
mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.” Warumi 4:4-5
Katika maneno hayo
tunaona kuwa neema ni kupewa usichostahiri kupewa, Kama kuna kitu umekifanyia
kazi, ujira wake sio neema kwako bali ni stahiri yako. Lakini kama hujafanyia
kazi hakuna unachostahiri, lakini ukipewa usichostahiri, kinahesabiwa kuwa
neema. Kwa kuwa anayetakiwa kupewa ni yule aliyestahiri au yule ambaye ni haki
yake, kwa hiyo neema inakutengezea mazingira au inakuweka mahali pa kustahiri
kupokea usichostahiri kupokea.
Kumbuka Mungu ni
mwenye haki, kwa hiyo humpa kila mtu anachostahiri. Kuna wakati tunakuwa mahali
ambapo hatuwezi kufikia vitu vingine, kwa hiyo anatumia neema kukuleta mahali
pa kustari ili kuweza kupokea. Mfano, mwanadamu alipoasi, alistahiri adhabu na
akaingia kwenye utumwa, kwa sababu hiyo alihitaji ukombozi. Nafasi yake ilikuwa
haipi kustahiri ukombozi huo. Ingawa Mungu aliweka tayari ukombozi huo, lakini
mwanadamu hakuwa kwenye nafasi ya kuupokea. Kwa hiyo Mungu anampa mtu neema
kumleta mahali pa kustahiri kupokea wokovu. Neema humpa mtu nafasi ya kuufikia
wokovu.
Kwa manane mengine
tunaweza kusema, neema ni fursa ya kulifikia jambo usiloweza kulifikia. Kila
ambacho huwezi kukifikia kwa kiinadamu, neema itakufikisha pale. Pale ambapo
matendo yako hayawezi kukufikisha, neema itakufikisha hapo.
“Kwa maana mmeokolewa
kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa
cha Mungu;” Waefeso 2:8
Mstari unatusaidia
kuelewa zaidi kuhusu neema. Kitu kisichotokana na nafsi zetu, juhudi zetu, lakini
tumepewa, kilichofanya tupokee ni neema. Na hiyo neema ni kipawa cha Mungu.
Kipawa hufanyii kazi kukipata bali hupewa bure. Inategemea huruma za yule
anayekupa.
KUJIFUNUA AU
KUDHIHILIKA KWA NEEMA
Imekuwa changamoto
kubwa pale ambapo Mungu anaachilia neema yake kwa mtu lakini huyo mtu anakuwa hajui kuwa neema
ya Mungu imeachiliwa juu yake. Hii ni kwa sababu kinachooneka kwa macho ni
matokea ya kutenda kazi kwa neema kuliko neema yenyewe. Watu wanapoona mambo
yanavyotokea wanashindwa kuelewa kuna kutenda kazi kwa neema nyuma yake. Mara
zote, unachokipokea sio neema bali kilichofanya hayo upokee ni neema. Kilichotokea
nyuma ya pazia ndio neema, ambayo inafanya kazi ya kufunua kitokee nje.
Hutumika neema kuvipokea vitu vya Mungu, kwa hiyo neema ndiyo inayotupa nafasi
kuvifikia vitu vya kimungu.
Neema hujifunua kwa
namna mbalimbali, la muhimu kujifunza ni kujua pale neema inapojifunua. Kutokana na
namna tofauti ambavyo neema hujifunua, tunaweza kuangalia kwa jumla namna
inavyojifunua.
a. Kupitia wema wake
“ili katika zamani
zinazokuja audhihirishe wingi wa
neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.” Waefeso
2:7
Biblia inasema, Mungu
audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi, na atafanya hivyo kwa njia ya wema wake. Neema ya Mungu hujfunua
kupia wema wa Mungu katika maisha ya mtu. Tunapoona wema wa Mungu maishani
mwetu, tunajua kwa hakika ni kujifunua kwa neema. Mungu ni mwema kwa wenye
dhambi na wasio na dhambi, anapowapo wema wake, sio kwamba wanastahiri lakini
kwa sababu ya kutenda kazi kwa neema yake. Anapowanyea mvua wenye haki na
waovu, ni udhirisho wa neema yake katika maisha ya hao watu.
Kujifunua kwa neema
kwa njia ya wema wa Mungu, ni pana sana kwa maana kwamba wema wa Mungu, inahusisha
karibia matendo yote ya Mungu anayoyafanya katika maisha yetu. Unapoona wema wa
Mungu unajifunua kwako, ujue Mungu anafunua wingi wa neema. mfano, upo kwenye mazingira ya kwamba unatakiwa kulipia malipo fulani muhimu na leo ndio siku ya mwisho kulipia, alafu unamwomba Mungu akufungulie mlango wa kupata pesa lakini mpaka jioni inafika hujapata pesa na bado hujui unapataje. lakini kesho inafika usikia mwisho wa kulipia umeongezwa mpaka baada ya siku mbili na kumbe siku hiyo ndiyo unapokea mshara wako unalipia malipo yako. Hiyo ni neema, katika wema wa Mungu ilikuwa katika Muda. Muda ndio uliobeba neema.
b. Kupitia ufahamu na maarifa
“Maana neema ya Mungu
iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo
yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na
haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;” Tito 2:11-12
Neema ya Mungu ili
ikuooe ni lazima ifunuliwe, isipofunuliwa inakuwa haina nguvu juu yako.
Mungu ni Mungu wa neema, na alikuwa na neema tangu mwanzo, lakini haikuweza
kutuokoa mpaka ulipofika wakati timilifu, alipoifunua hiyo neema kwetu na sasa
tunaokolewa kwa hiyo neema. Na hiyo neema hujifunua kwa kuachilia ufahamu na maarifa ndani yatu juu ya
kile ambacho Mungu anataka kukuokoa. Ona neno hili, “…..nayo yatufundisha……’
Sio tu neema, bali neema iliyofunuliwa. Neema ikifunuliwa juu yako, inaachila
mwangaza juu ya namna ya kufanya na kushughurikia jambo fulani.
Mungu akaitaka
kukusaidia juu ya jambo fulani, anaachilia neema yake itakayokupa ufahamu namna
ya kushughurikia jambo hilo. Mfano, Biblia inasema “iko njia ionekanayo kuwa
sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti” (Mithali 14:12) Kuna njia unaweza ukawa
umechukua na usijuae kuwa umekosea kabisa. Katika kukusaidia, Mungu anaachilia na
kufunua neema yake kwako ambayo itakupa ufahamu juu ya mahali ulipo na
unakotakiwa kwenda. Gafla ndani yako unapata ufahamu ndani yako kuwa jambo
unalolifanya sio sahihi. Baada ya hapo kazi inakuwa kwako, kurudi ama kuendelea
hivyo hivyo.
Mungu anapokupa
maarifa na ufahamu juu ya ufalme ujue neema yake imefunuliwa kwako, ili uweze
kwenda sawa na huo ufahamu. Kuna wakati ambao Mungu huachilia neema yake, na
kukupa nafasi ya kufikia sehemu fulani ya maarifa, ikiwa na maana anakuhitaji
mahali kwa utumishi. Ile neema inakuwa dhahiri kwako na kujua wapi unakoelekea.
Nafasi ya kupata maarifa na ufahamu fulani inakuja kwa sababu ya neema iliyofunuliwa
ndani yako, na hii inakuwa ishara kuwa Mungu anakupeleka mahali fulani. Mungu
anakupa nafasi ya kujiendeleza kielimu na kuongeza maarifa, hiyo nafasi huja
kwa neema inayoachiliwa kwako kwa sababu iko nafasi inayokusubiri.
“Rehema na kweli
zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya
mwanadamu.” Mithali 3:3-4
“Mwanangu, yasikilize
mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako, Kwa maana hayo
yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako.” Mithali
1:8-9
Kwa maneno mengine
mithali inatuambia fursa ya kupata mafundisho na kusikia sheria ni udhihirisho
wa neema, Mafundisho hayo na sheria yanatengeza nafasi ya kushughurikia
ipasavya mambo yaliyoko mbele yako. Njia pekee ya ushughurikia jambo linapokuwa
ni kupata ufahamu na maarifa, neema ya Mungu kufunuliwa kufungua njia hiyo kwa
kukupa maarifa na ufahamu ili uweze kushughurikia hilo swala.
c. kupitia mambo/matendo yanayofanyika
“Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao,
watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana. Habari hizo za watu hao zikafika
masikioni mwa kanisa lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba, aende
hata Antiokia. Naye, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi,
akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.” Matendo 11:21-23
Jambo la muhimu kujua ni kuwa
neema huonekana. Baada ya Barnaba kufika Antiokia, alifanikiwa kuona neema ya
Mungu kwa watu, akafurahi. Barnaba alifanikiwa kuiona neema hiyo ya Mungu kwa
kuangalia mambo au matenda ambayo yalikuwa yanafanyika huko Antiokia. Biblia
inasema, mkono wa Bwana ukawa pamoja na mitume, wengi wakamwelekea Bwana kwa
kumwamini. Alipoyaona matendo yaliyokuwa yakiendelea kufanyika, akaona neema. Ikiwa
na maana kuwa yale matendo yalikuwa yanafunua neema ya Mungu kiasi ambacho anaweza
akaona hiyo neema katika matendo. Kupitia matendo yanayofanyika una uwezo wa kuona
neema iliyo juu ya mtu, watu, eneo au juu yako.
Mfano, ingawa neema ya Mungu
ilikuwa haitajwi mara kwa mara katika agano la kale lakini matendo amboyo Mungu
alikuwa anafanya, yalikuwa ni matendo ya neema. Kwa kuangalia jinsi Mungu alipokuwa
akibakisha mabaki ya watu wakati walistahiri kuangamizwa taifa lote. Kupitia hii
unaona neema ambayo Mungu alikuwa anaachilia kwa taifa.
Kwa mfano, biblia inasema hivi:-
“Bwana asema hivi,
Watu wale walioachwa na upanga walipata neema jangwani; yaani, Israeli,
hapo nilipokwenda kumstarehesha.” Yeremia 31:2
Ingawa Mungu alitaka
kuwaangamiza wote, lakini neema yake ilifanya asiangamize wote bali abakishe
mabaki. Hayo mabaki yaliyosalia yalitokana na neema iliyoachiliwa juu ya taifa
ili kuwaokoa lasivyo taifa lote lingefutiliwa mbali.
Itaendelea, fuatilia mfululizo huu
Itaendelea, fuatilia
muendelezo
NEEMA YA MUNGU INAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUSHINDA MAJARIBU NA KUISHI MAISHA YA USHINDI KATIKA ULIMWENGU HUU-3
Reviewed by Unknown
on
2:18:00 PM
Rating:

Asante kwa somo kuhusu Neema, Mungu awabariki.
ReplyDeleteAsante kwa somo kuhusu Neema, Mungu awabariki.
ReplyDeleteUzidi kubarikiwa na MUNGU Amin.
ReplyDelete