BREAKING NEWS

[5]

NEEMA YA MUNGU INAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUSHINDA MAJARIBU NA KUISHI MAISHA YA USHINDI KATIKA ULIMWENGU HUU -2



NEEMA YA MUNGU INAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUSHINDA MAJARIBU NA KUISHI MAISHA YA USHINDI KATIKA ULIMWENGU HUU-2



Tuendelee kujifunza kuhusu somo letu katika sehemu ya pili.


Tuliishia mahali kwamba, ni utamaduni sasa kuwaa kijana ni lazima awe na mpenzi wake wa jinsia tofauti hata kama bado hajafikia umri wa kuoa au kuolewa. Watoto wanazaliwa na kukukua katika kawaida hiyo, wakiona ni jambo jema nao wanaliendeleza. Ni hafadhari ya nchi za Afrika, lakini nchi za ulaya na nchi za magharibi ni ukweli mtupu katika jambo hili.

Ukweli ni kwamba watu wa jamii humkubali na humpokea kwa furaha mtu yule  anayekubaliana na mfumo na utamaduni wao. Kwa sababu mifumo miwili ni vigumu kufanya kazi katika sehemu moja. Watu wa jamii hiyo wanautambua mfumo na utamaduni wao tu katika nafsi zao, kufanyika kwa jambo lolote lililotofauti na utamaduni wao ni hakika kwamba watalipinga na kulifutilia mbali.

Isaya 59:15 inasema “Naam, kweli imepungua kabisa, naye auchukiaye uovu ajifanya kuwa mateka, naye BWANA akaona hayo, akachukizwa kwa kuwa hapana hukumu ya haki”. Ukisoma kuanzia mstari wa kwanza wa sura hii utaona wazi aina ya mfumo na utamaduni uliokuwa katika jamii ya watu wale, mambo ya giza yaliyokuwa yakifanywa nao kiasi ambacho yeye aliyeuchukia uovu uliokuwa unafanywa, alijikuta ni mhanga wa kuchukia uovu. Jamii ya watu wale walikuwa wanaona ni kubadilishiwa mfumo waliouzoea na ili kumfutilia mbali na kumkomesha ni kumpinga kwa kumtengenezea jambo baya yeye achukiaye uovu. Hakika ndio mambo tuliyonayo kwenye nchi yetu pia na sehemu mbalimbali za dunia, mtu apendaye haki na kufuata kweli ndiye aangamiaye. Yeye akataaye kutoa au kupokea rushwa ndiye atengenezewaye kesi ya wizi na kufungwa jera, yeye atoaye taarifa za madawa ya kulevya ndiye mhanga wa kifo kwa sababu rushwa imeshakuwa mfumo na utamaduni kwa sasa katika sehemu mbalimbali za nchi yetu. Watoto wanazaliwa, wanakuwa katika mfumo na utamaduni wa rushwa na kuiendeleza.

Kufanya mabadiliko ya mfumo na utamaduni ambao ulimwengu umezoe sio kazi nyepesi kwa sababu ulimwengu huo utasimama kwa nguvu zote kuhakikisha utamaduni waliouzoea unaendelea kubaki na kudumishwa. Yesu alisema kwamba “Nami nitamwomba baba naye atawapa msaidizi mwingine,………ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui,…..” ulimwengu  hauwezi kumpokea kwa sababu ya mfumo wa maisha mpya ambao Roho mtakatifu anao ambao hautambuliki kwa ulimwengu. Roho mtakatifu angeweza kupokelewa kwa furaha kama angekuwa na mfumo mmoja wa maisha na ulimwengu. Ile kwamba Roho mtakatifu haendani na mfumo na utamaduni wa ulimwengu kumpokea kungemaanisha kuharibiwa kwa utamaduni wao jambo ambalo wasingependa litokee kwa hiyo kinachofanywa ni kumkaata na kumpinga.

Ulimwengu huu wote wa sasa ndivyo ulivyo, unaenenda kinyume na Mungu aliyeumba mbingu na nchi, biblia inasema “Toka mbinguni Mungu aliwachungulia wanadamu, aone kama yuko mtu mwenye akili, amtafutaye Mungu, kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja, hakuna hatendaye mema La! Hata mmoja (Zaburi 53:2-3), hali hii ni ya kawaida kwa watu wa ulimwengu na wameizoea. Sio rahisi kabisa kuishi vizuri ukiwa na tofauti na kawaida hii. Inapotokea mtu anataka kuishi tofauti na hiyo kawaida, ndipo adha, dhiki, mateso, majaribu na shida zinapotokea kwa huyo mtu. Wakati kundi kubwa la watu wasemapo “ndiyo” peke yako ndiye uliye na jibu la “hapana”. Wakati wote wakisema ndoa ya jinsia moja ihalalishwe, peke yako tu unajibu la kupinga na kusimamia maamuzi yako. Shida inakuja je uko tayari kusema na kusimamia maamuzi yako unapojikuta uko peke yako? Na Mungu anataka nini?

Tuangalie mfano mmoja kwenye biblia katika Yeremia 23:25-28, maandiko yanasema

“Nimesikia waliyoyasema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema nimeota ndoto, nimeota ndoto. Je! Mambo hayo yatakuwa katika moyo wa manabii wanaotabir uongo hata lini, manabii hao wenye udanganyifu katika mioyo yao wenyewe? Wanaodhani watawasahaulisha watu wangu jina langu kwa ndoto zao, wanazomhadithia kila mtu na jirani yake, kama vile baba zao walivyolisahau jina langu kwa ajili ya baali. Nabii aliye na ndoto na aseme ndoto yake na yeye aliye na neno langu na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema BWANA”      

Haya yalikuwa ni maneno ya Mungu kwa kinywa cha nabii Yeremia, kwenda kwa wana wa Israeli kuhusiana na manabii wao waliokuwa wanatabiri uongo na kuwatumainisha kwa amani mambo ambayo hayako wala hayatatokea. Manabii wote isipokuwa Yeremia walikuwa wa uongo wakitabili uongo ili kuwasahaulisha watu jina la BWANA na watu waliambatana nao na kuwapenda. Wakati manabii wote walisema kuna amani na watu wakawaamini na kuambatana nao Yeremia anapokea neno la BWANA kwamba hakuna amani, (Yeremia 23:17-21). Katika mazingira kama hayo, wakati taifa zima limeambatana na hao manabii, Yeremia akapokea jibu la tofauti, je, ingekuwawewe ndiye uliye na jibu tofauti utapata nguvu ya kusema neno lako? Nguvu na ujasiri unautoa wapi? Je nawe hautaweza kujiunga na msimamo wao na kuuacha wa kwako? Maana ni rahisi kukataa lakini matokeo yake ni magumu. Yeremia alikuwa akiteswa, akipigwa, akifungwa minyororo na kuwekwa gerezani kwa sababu ya kusema neno la BWANA lililo kinyume na matakwa yao, (Yeremia 26:8,11). 

Katika mazingira kama hayo, hata kwa mateso, magumu, adha na shida bado Mungu anasema “Nabii aliye na ndoto na aseme ndoto yake na yeye aliye na neno langu na aseme neno langu kwa uaminifu”. Hata kama itagharimu maisha, maadamu una neno lake ndani, Mungu anahitaji uliseme na kulifanya kwa uaminifu. Kwa maneno mengine Mungu anatazamia ushindi katika mazingira kama haya tukiwa na nguvu na ujasiri kusema na kufanya mambo yake kwa uaminifu. Ndio maana maandiko yanasema "Mtumikieni BWANA kwa kicho, shangilieni kwa kutetemeka" (Zaburi 2:11). Inagharimu hofu ya Mungu kuua/kuondoa hofu ya vitu au watu wengine ndani yako.

Mungu hataki uanze kuushutumu ulimwengu kwa jinsi ulivyo bali anatazaamia uyaishi maisha ya Kristo Yesu ndani yake kwa ushindi bila kuteteleka.

Ni ninalotaka ujue ni kuwa ulimwengu huu upo kinyume kabisa kimwenendo na namna ambavyo Mungu anataka, lakini bado anataka kwamba Tuuishi mwenendo wetu kama tulivyoupokea katika Kristo.

Mungu anajua hali halisi ya dunia. Anajua adha, shida, dhiki, mateso ambayo ulimwengu ulionao hasakwa wale ambao kwa wale ambao wameambua kwenda kinyume cha ulimwengu huo.

Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa”. 2Timothy 3:12

Kila anayependa na kutaka kuishi maisha ya utauwa, ni lazima ataudhiwa, kwa hiyo ni muhimu ajiandaa kwa ajili ya dhiki, adha na maudhi yatakapokuja. Yesu pia anajua hali ya dunia jinsi ilivya na akatutia moyo, akasema “………Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”. (John 16:33) Kwa hiyo unapokutana na dhiki na shida, unahitaji kuelewa kuwa ni hali ya dunia, ukifika mbinguni hautakutana na mambo haya.

Swali la ujiuliza, ninaweza kuishi katika mazingira haya kwa ushindi na katika mapenzi ya Mungu. Kama Mungu anajua hali ya ulimwengu huu, hawezi akawa ametuacha hivi hivi bila msaada wa namna ambavyo tunaweza kuishi katika Kristo kwa ushindi. Kuna mengi ambayo Mungu ameyafanya kuhakikisha kwamba tunaishi kwa ushindi katika ulimwengu huu wa sasa. Kimoja wapo ni kutupa neema yake-NEEMA YA MUNGU.

Asante kwa kusoma, tutaendelea na mfululizo wetu.
NEEMA YA MUNGU INAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUSHINDA MAJARIBU NA KUISHI MAISHA YA USHINDI KATIKA ULIMWENGU HUU -2 NEEMA YA MUNGU INAVYOWEZA KUKUSAIDIA KUSHINDA MAJARIBU NA KUISHI MAISHA YA USHINDI KATIKA ULIMWENGU HUU -2 Reviewed by Unknown on 9:08:00 AM Rating: 5

1 comment:

  1. Aksanti kwa somo nafurahi sana na nimebarikiwa sana

    ReplyDelete

Sora Templates