BREAKING NEWS

[5]

JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-3




    JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-3

Neno la Kusimamia.
Mithali 4;23  "Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima
Karibu tuendelee kujifunza jinsi ya Kulinda Moyo,leo tutamalizia somo letu hili.
 
Tatazame maandiko kidogo kuhusu macho yako.
Kama tulivyokwisha kuona hapo juu kuwa macho yako ni kinywa cha moyo wako, ukilitambua hili Hutakuwa mpumbafu na kula kila kitu.Huwezi ukaanglia kila kitu kwasababu unapoangalia wewe unafikiri unaangalia lakini ukweli ni kwamba moyo wako unakuwa unakula.

,Habakuki 1;13. Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu,

Maneno ya Habakuki akizitaja sifa za Bwana Mtakatifu wa Israel, anazungumza juu ya Mungu kuwa na Macho matakatifu kiasi ambacho hawezi kuutazama Uovu. Mungu ni mtakatifu sana na Utakatifu huo ndio Habakuki anausemea kama Usafi wa macho ambao kwa jinsi ulivyo mkuu sana macho yake hayawezi kutazama Uovu,Neno la Mungu linasema Mungu anakaa ndani yetu na Zaidi Mungu alisema Nanyi mtakuwa Watakatifu kwa kuwa mimi ni Mtakatifu,sasa jaribu kufikiri huyu Mungu aliyemtakatifu asiyeweza kutazama Uovu anaishi ndani ya Moyo wako,na amesema wewe wapaswa kuwa Mtakatifu kama yeye,Utakatifu huo ndio uliomfanya asiweze kutazama Uovu.Mtu aliyeokoka hawezi kutazama kila kitu maana Mungu aliyendani yake hawezi kutazama kila kitu.

Kwasababu ya kukosa Ufahamu huu wana wengi wa Mungu wameeangamia na hata sasa wanaangamia na cha ajabu ni kuwa hata wengine wanatetea juu ya vyakula wanavyokula(Vitu wanavyovisikiliza na wanavyovitazama).Kinachosikitisha na kushangaza ni kuona jinsi watu wanavyokuwa waangalifu juu ya aina ya vyakula na vinywaji wanavyomlisha mtu wa nje,utasikia mtu akikwambia nina aleji na Maharage,ooohh soda nyeusi ni mbaya kwa afya yangu,wapo watu wasiokula baadhi ya vyakula kwasababu tu kwao vinaonekana vyakula rahisi yaani vyakula vya kimaskini kwa lugh ya wazungu utawasikia wakisema “This food is too cheap,this kind of food is not my type” wao kul ugali kwao ni kujishusha thamani.Watazame Waimbaji wanavyochagua vyakula na vinywaji na juhudi hizi zote ni kwa ajili ya mtu wa nje ambaye ni mavumbi asiye wa kudumu.Lakini mtu wa ndani(moyo) ambaye ni wa kudumu huyo hapewi thamani,huyo anaonekana anastahili kula kila kitu hata kama ni sumu huyo wanamlisha tu wasichokijua ni kwamba ni bora Sumu anayokula mtu wa nje ambaye anaweza tu kupewa mziwa kwa dakika chache sumu ikatoka akawa mzima au kwa kuwekewa drip ya maji na damu yake ikawa safi,tofauti na sumu anapopewa ntu wa ndani ni hatari sana,gharama ya kuiondoa hiyo sumu na madhara yake ni kubwa sana na inaweza kuchukua miaka kuindoa hiyo sumu kwenye moyo wa mtu.Watu waliowahi kula sumu ya picha za uchi “phonograph”  (ndio nasema Sumu ili kila alaye ajue anajiua mwenyewe)na sasa wameokoka wanaweza kushuhudia vizuri gharama waliyolipa na pengine bado hata sasa wanalipa kwa kupitia Utakaso wa Neno la Mungu ambalo ni Maziwa yasiyoghushiwa ili kuitakasa mioyo yao na kuiondoa hiyo sumu ndani ya mioyo yao.
Waefeso 5;25-27.
“Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa

Neno hili limekuja kwa lengo la kukupa ufahamu utaobadilisha mfumo wa maisha yako ambao huo umekuwa ukiharibu moyo wako na matokeo yake badala ya moyo kububujika maneno yenye munyu na mawazo mema unabubujika matusi,mawazo ya tamaa na uzinzi.

Moyo wako ni wa thamani sana Uhai wako unategemea hali ya huyo mtu wa ndani,kama vile unavyoweza kusema This kind of food is not my type kwa ajili ya mwili vivyo hivyo mtu wa ndani ni wa thamani sana,,,not every kind of food is worth feeding him,,remember only a fool feeds on trash.Acha kula jalalani.Be selective acha kuangalia miziki ya kidunia inayoutukuza Uzinzi na kuwasha moto wa tamaa ndani yako.Acha kuwa na kiburi kwa kusema kwani kusikiliza huo muziki kunashida gani,husikilizi unakula.

Acha kunywa sumu ya phonograph maana hakika utakufa, Ni sumu ya hatari sana ni sawa na wadudu wanaokula mizizi ya mti baada ya muda mti utaanguka pasipo watu kujua.Ni dhambi inayoshambulia maisha yako ya sirini, huko ambako ndiko ulipaswa kukitaa mizizi ya maisha ya Utakatifu.

Vijana wengi walio ndani ya kanisa na walio nje wapo kwenye gereza hili. Na ubaya wa gereza hili ni kwamba ni gereza la Sirini.Pasipo mfungwa mwenyewe kuamua kutafuta msaada hakuna mtu anayeweza kujua kuwa mpendwa yupo gerezani.

Kama tayari upo kwenye gereza la picha hizi za Uchi zinzojazaa Uchafu kwenye moyo wako, tafuta msaada wa Yesu Kristo ili utoke hapo.
Kwasababu sio vita unayoweza kutoka mwenyewe pasipo msaada wa Mungu.

Tafuta Mtumshi wa Mungu aliyehai ambaye ndani yako unasikia amani kusema naye,ili kwa pamoja mvipige vita hivyo ili utoke hapo.Uwe huru kwa maana ni hakika kila atazamaye Uchafu huu ni mtumwa wa Ibilisi.Nyuma ya hizo picha ipo roho iliyokufunga ndio maana jitihada zako za kuacha zinafeli kila siku.Ni mpaka Roho yenye nguvu (Roho ya Yesu) kuliko hiyo roho iingilie kati ndio unaweza kutoka kwenye gereza hilo la picha za ngono linaloharibu moyo wako.

Yohana 8:34
Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.

2Peter 2:19
 wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule.


Acha kuambatana na marifiki ambao stori zao ni kuhusu uzinzi, uchafu na tamaa.

Linda moyo wako linda uzima wako, kama ulishaharibika Urudishe kwa aliyeufinyanga aufinyange upya, kwa Roho Mtakatifu kwa maji katika Neno lake.


Neema ya Yesu Kristo iwe juu yako kukuwezesha kuliishi neno hili na hatimaye kufanikiwa kuulinda moyo wako ili Uzima uzidi kububujika kinywani mwako kutoka kwenye moyo wako.

JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-3    JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-3 Reviewed by Unknown on 5:43:00 PM Rating: 5

6 comments:

  1. Somo zuri sana hili nimebarikiwa sana

    ReplyDelete
  2. Good message🙏🙏🙏

    ReplyDelete
  3. Thank you for the word of God, be blessed 🙏

    ReplyDelete
  4. Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

    Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

    Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

    Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

    Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

    Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159
    dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete
  5. Uchawi wa mapenzi wa Dkt. Dawn hufanya maajabu kweli.

    Niliwasiliana na Dkt. Dawn wakati uhusiano wangu ulipovunjika kabisa. Mpenzi wangu wa zamani alikuwa ameniacha na kunizuia kwenye mitandao yote ya kijamii. Nilivunjika moyo na kupoteza tumaini. Baada ya kushauriana na Dkt. Dawn, kila kitu kilibadilika. Mpenzi wangu wa zamani alirudi peke yake, akaomba msamaha kwa dhati, na akaomba msamaha. Leo, tunaishi pamoja kwa furaha, na hata tuna mtoto.

    Maneno hayatoshi kuelezea jinsi ninavyoshukuru. Kutokana na uzoefu wangu, naweza kusema kwa ujasiri kwamba Dkt. Dawn ni halisi, anayetegemewa, na mwenye nguvu. Ikiwa unakabiliwa na hali yoyote ngumu maishani mwako hivi sasa, Dkt. Dawn anaweza kukusaidia.
    ANAWEZA KUKUSAIDIA KWA MATATIZO YAFUATAYO:
    Kurudisha ndoa na mahusiano yaliyovunjika
    Kuvutia mafanikio na ukuaji katika biashara
    Matatizo ya uanaume, utasa, na ukosefu wa watoto
    Kurejesha mali zilizoibiwa au zilizopotea
    Kurudisha kazi zilizopotea au fursa za kazi
    Kinga dhidi ya uchawi na macho mabaya
    Hirizi za mvuto
    Kutatua migogoro ya ardhi na mali
    Kuwafanya wapenzi kutimiza ahadi zao
    Kushinda kesi mahakamani, na mengine mengi
    Huu si ulaghai — ni ushuhuda kutoka kwa uzoefu.
    Kwa maelezo zaidi, wasiliana naye moja kwa moja kwenye WhatsApp. +2349046229159
    dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete

Sora Templates