JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2

JINSI YA
KULINDA MOYO WAKO-2
Neno la Kusimamia.
Mithali 4;23 "Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima”
Karibu tuendelee kujifunza jinsi ya Kulinda Moyo, leo tunaendelea
kwa Kuangalia Vinywa vya Moyo ambavyo kwa hivyo Moyo wa mtu Hula.
Vinywa vya Moyo
- Macho.
Macho ni mdomo wa
moyo, chochote kiingiacho kwa macho hicho huenda moja kwa moja kwenye moyo na
hicho ndicho kiwezacho kuutia moyo Unajisi.Mtu anapokuwa anatazama kwa macho
yake anakuwa anakula, yaani anamlisha mtu wa ndani (moyo wake).Yesu alisema mtu
mwema kutoka kwenye akiba njema na mtu mwovu kutoka kwenye akiba mbovu, hapo
juu nimekwambia kuwa Akiba hukaa ghalani na akiba haijii automatically kwenye
ghala, bali huwekwa ghalani na ndipo baadae hutoka.
Tuangalie kwenye
Mithali Jinsi akiba inavyotengenezwa ndani ya moyo na baadae itadhihirika.Weka
ili moyoni kuwa kuna milango ambayo kwa hiyo kilichoko moyoni hutoka nje,na
kinachoamua sio mlango unaotoa bali ghala ambayo hapa ni Moyo.
Mithali 15;2,
2
Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu
humwaga upumbavu
Mithali 15;14
14
Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa; Bali kinywa cha wapumbavu hula
upumbavu
Maneno haya ni
yaajabu sana,na yanatupa Hekima ya ajabu sana ambayo kwa hiyo tutaweza kulinda
moyo,Mhubiri anasema Hekima ni Ulinzi kwa aliyenayo.,tuendelee kula Hekima hii
kwa pamoja,maana hata hapa unakula.
Mstari wa 2a
unatuonyesha kuwa Ulimi wa mwenye Hekima hutamka maarifa.Kulingana na Neno la
Yesu kuwa kinywa cha mtu hayanena yote yaliyo moyoni mwake,tunaweza kutambua
kuwa Ulimi huu unamwaga Hekima lakini Hekima hii haitoki kwenye kinywa bali
inatoka ghalani yaani moyoni,kuelewa Zaidi tujiulize Hekima hii ilifikaje
Moyoni?
,Mstari wa 14a
Unatupa majibu mazuri kuwa Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta
maaraifa,ukiunganisha mistari hii miwili utapata tafsiri hii..mwenye Hekima
alitafuta maarifa kwa bidii na hekima hiyo ikakaa moyoni mwake na baadae kwa
Ulimi wake alitamka au kurelease akiba iliyokuwa moyoni mwake.mahali pengine
kwenye mithali anasema Moyo wa mwenye hekima hufundisha kinywa chake na
kuzidisha elimu ya midomo yake.(Mithali 16;23).
Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa
chake; Huzidisha elimu ya midomo yake.
Tukirudi kwenye
Mistari hii sehemu b,Mstari wa 2b unasema Bali
vinywa vya wpumbafu humwaga Upumbavu na 14b inasema Bali kinywa cha wapumbafu hula Upumbafu..sasa utaona kwenye mistari
yote kuna Neno kinywa,kimoja kinamwaga yaani kunaachilia Upumbavu na kimoja
kinakula,,Usichanganye Vinywa hivi ni Vinywa viwili tofauti,Kinywa kinachomwaga
Upumbavu huu ni mdomo unaonena yaliyoko moyoni,na mdomo unakula Upumbafu huu
ndio mdomo wa moyo (macho) ambao huu sasa ndio unaopeleka chakula kwenye
moyo.Ukichanganya mistari hii miwili utaona kuwa Upumbafu Unaliwa kwa Kinywa
cha moyo ambacho hapa ni macho. Upumbafu huu huifadhiwa moyoni na baadae
humwaga kwa kinywa.Biblia ya kingereza inasema.. but the mouth of fools feeds on foolishness. (AKJV).Kinywa cha
mpumbafu hula Upumbafu,”only the fool feed on trash.”
Kutokujua haya kumefanya wengi kutazama kila
kitu pasipo kujua kuwa wanapotazam ndipo moyo wao unakula.Hivyo wengi
wamejikuta wakitamka na kutenda mambo maovu pasipokujua kuwa wao wenyewe ndio
waliojitengenezea hayo mambo mioyoni mwao.Kama moyo wako unahitaji kalinda
Utakatifu basi sio kila kitu kinafaa kuangaliwa na wewe,kwa maana
unachokiangalia kinaweza kutia moyo wako unajisi.
Mithali 23;33
Macho
yako yataona mambo mageni;Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
Neno la msingi hapa ni mambo Mageni,Lazima
mtu ajiulize Mambo mageni ni mambo ya namna gani hata yaweze kusababisha moyo
wa yule anayetazama utoe mambo yaliyopotoka.
Kwa vyovyote vile mambo haya lazima yatakuwa
yamepotoka na ndio maana matokeo yake ni akiba ya Uovu moyoni mwa aliyeona.
Neno la Mungu linasema(Kumbu 32;12) Wala
msiabudu miungu wageni.Maana yake mambo mageni ni mambo yanayohusu miungu
wageni.Maana yake mtu anapotazama vitu vyote vya mungu megini ambaye ni Ibilisi
matokeo yake ni Moyo wake kutoa yaliyopotoka. Hii inakupa kuona kuwa wakati mtu
anapokuwa anatazama mambo haya alikuwa anaweka akiba kwenye moyo wake akiba
iliyopotoka na ndio itakuja kudhihirika baadae.Maana yake chochote
anachokitazama mtu kama anayetukuzwa hapo ni mungu megeni au Ibilisi tarajia
kabisa moyo wake kutoa Maovu baadaye.
Kumbukumbu 32:12
“Bwana
peke yake alimwongoza, Wala hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye”
2.Sikio
Sikio lako ni Kinywa cha moyo wako..Ukisoma maneno ya Ayubu
utashangaa kidogo kukuta maneno haya juu ya sikio,,Ayubu 12;11 “Je sikio haliyajaribu maneno kama Ulimi
uonjavyo chakula” Ulimi huonja chakula na kamwe hautakula chakula kilicho
kichungu labda tu iwe ni dawa,ndivyo hivyo Sikio nalo huyajaribu maneno,Kwanini
linayajaribu ? Hii ni kwasababu sio kila chakula kinafaa kwa afya ya moyo vipo
vingine ni sumu na vikiruhusiwa tu kuingia basi moyo utaharibika.
Ukisoma 1Corinto 15;33..Utakutana na maneno haya “Msidanganyike;Mazungumzo mabaya huharibu
tabia njema..Tabia ni matunda ya hali ya moyo, hivyo njia pekee ya
Mazungumzo kuweza kuharibu Tabia njema ni kama hayo mazungumzo yanaweza
kuathiri asili ya mti yaani moyo.Tabia njema ni matokeo ya akiba njema
iliyondani ya moyo wa mtu.Hivyo kama mtu mwema ataanza kuweka akiba mbovu ndani
ya moyo wake baasi baada ya muda tabia mbaya ndiyo itakayodhihirika kwasababu
mtu mwovu kutoka kwenye akiba mbovu hutoa maovu.Na Roho Mtakatifu anaonya
kabisa kuwa Tusidanganyike mazungumzo mabaya huharibu tabia njema lazima
tuelewe jambo hili kuwa maneno haya mabaya yanaingia kwenye moyo na baada ya
muda yanaanza kudhihirika nje kwa kinywa au matendo.
Waefeso 5;3-5.inazungumza juu ya kuonya watakatifu kuwa Uasherati
usitajwe kwao,yaani haiwapasi watakatifu kuwa na mazungumzo yanayohusu
uasherati,,na agizo hili sio juu ya kufanya Uasherati bali ni juu ya
Kuuzungumzia,baada ya kutafakari sana Roho Mtakatifu akanionyesha kwanini Alionya
kuhusu Uasherati kutajwa(kuzungumzwa na watakatifu).Ukiangalia maneno hayo
Utaona katazo la kutaja mambo ya Uasherati mstari wa 3 halafu mstari wa
5..anasema Maana mnajua Waasherati hawataa urithi Ufalme wa Mungu,,sasa waweza
kujiuliza kwani kuzungumzia mambo ya Uasherati na Mwasherati vinamahusiano
gani.Lakini Waasherati wanaotajwa mstari wa 5 wanatengenezwa na mazunguzo ya Uasherati
waliyokuwa wanayataja hapo kwenye mstari wa 3 walipokuwa watakatifu.Maneno
yanaumba tabia ndani ya mtu hivyo Mtakatifu akiendelea kusikiliza na
kujihusisha na mazungumzo ya Uasherati baaada ya muda atakuwa
mwasherati.Mazungumzo unayoyasikiliza yanakuumbaa uwe mtu wa aina ya mazungumzo
unayoyasikiliza.Unaweza usione madhara mwanzoni lakini Neno la Mungu
limehakikishwa baada ya muda utakuwa kama marafiki unaoombatana nao kwakusiliza
mazungumzo yao.Maana wanapozungumza wewe unakula.Angalia sana watu unaoshiriki
nao ni kama hotel unayokula,kama wanazungumza maneno machafu basi ujue unakula
jalalani na baada ya muda uchafu utatoka kwenye moyo wako.Wapumbavu tu ndio
hula jalalani.
Waefeso 5;3-5 Lakini
uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama
iwastahilivyo watakatifu;wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo
hayapendezi; bali afadhali kushukuru.Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba
hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na
urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na
maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi. Basi
msishirikiane nao.”
Naamini umepata kitu
cha kukusaidia kuulinda moyo wako.Tutaendelea Mungu akitupa Neema yake katika
Kristo Yesu Bwana wetu.
Amani na Neema
zitokazo kwa Bwana Yesu ziwe kwako.
JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2
Reviewed by Unknown
on
6:02:00 PM
Rating:

Nimebarikiwa sana ....Mungu akutie nguvu
ReplyDeleteGod Bless you I am blessed
ReplyDeleteBarikiwa Maana wa Mungu,nimejifunza kiti
ReplyDelete