BREAKING NEWS

[5]

JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2



    JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2

Neno la Kusimamia.
Mithali 4;23  "Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima”
Karibu tuendelee kujifunza jinsi ya Kulinda Moyo, leo tunaendelea kwa Kuangalia Vinywa vya Moyo ambavyo kwa hivyo Moyo wa mtu Hula.
 
Vinywa vya Moyo

  1. Macho.
Macho ni mdomo wa moyo, chochote kiingiacho kwa macho hicho huenda moja kwa moja kwenye moyo na hicho ndicho kiwezacho kuutia moyo Unajisi.Mtu anapokuwa anatazama kwa macho yake anakuwa anakula, yaani anamlisha mtu wa ndani (moyo wake).Yesu alisema mtu mwema kutoka kwenye akiba njema na mtu mwovu kutoka kwenye akiba mbovu, hapo juu nimekwambia kuwa Akiba hukaa ghalani na akiba haijii automatically kwenye ghala, bali huwekwa ghalani na ndipo baadae hutoka.

Tuangalie kwenye Mithali Jinsi akiba inavyotengenezwa ndani ya moyo na baadae itadhihirika.Weka ili moyoni kuwa kuna milango ambayo kwa hiyo kilichoko moyoni hutoka nje,na kinachoamua sio mlango unaotoa bali ghala ambayo hapa ni Moyo.

Mithali 15;2,
2 Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu

Mithali 15;14
14 Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa; Bali kinywa cha wapumbavu hula upumbavu

Maneno haya ni yaajabu sana,na yanatupa Hekima ya ajabu sana ambayo kwa hiyo tutaweza kulinda moyo,Mhubiri anasema Hekima ni Ulinzi kwa aliyenayo.,tuendelee kula Hekima hii kwa pamoja,maana hata hapa unakula.

Mstari wa 2a unatuonyesha kuwa Ulimi wa mwenye Hekima hutamka maarifa.Kulingana na Neno la Yesu kuwa kinywa cha mtu hayanena yote yaliyo moyoni mwake,tunaweza kutambua kuwa Ulimi huu unamwaga Hekima lakini Hekima hii haitoki kwenye kinywa bali inatoka ghalani yaani moyoni,kuelewa Zaidi tujiulize Hekima hii ilifikaje Moyoni?
,Mstari wa 14a Unatupa majibu mazuri kuwa Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maaraifa,ukiunganisha mistari hii miwili utapata tafsiri hii..mwenye Hekima alitafuta maarifa kwa bidii na hekima hiyo ikakaa moyoni mwake na baadae kwa Ulimi wake alitamka au kurelease akiba iliyokuwa moyoni mwake.mahali pengine kwenye mithali anasema Moyo wa mwenye hekima hufundisha kinywa chake na kuzidisha elimu ya midomo yake.(Mithali 16;23).
Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake; Huzidisha elimu ya midomo yake.


Tukirudi kwenye Mistari hii sehemu b,Mstari wa 2b unasema Bali vinywa vya wpumbafu humwaga Upumbavu na 14b inasema Bali kinywa cha wapumbafu hula Upumbafu..sasa utaona kwenye mistari yote kuna Neno kinywa,kimoja kinamwaga yaani kunaachilia Upumbavu na kimoja kinakula,,Usichanganye Vinywa hivi ni Vinywa viwili tofauti,Kinywa kinachomwaga Upumbavu huu ni mdomo unaonena yaliyoko moyoni,na mdomo unakula Upumbafu huu ndio mdomo wa moyo (macho) ambao huu sasa ndio unaopeleka chakula kwenye moyo.Ukichanganya mistari hii miwili utaona kuwa Upumbafu Unaliwa kwa Kinywa cha moyo ambacho hapa ni macho. Upumbafu huu huifadhiwa moyoni na baadae humwaga kwa kinywa.Biblia ya kingereza inasema.. but the mouth of fools feeds on foolishness. (AKJV).Kinywa cha mpumbafu hula Upumbafu,”only the fool feed on trash.”
Kutokujua haya kumefanya wengi kutazama kila kitu pasipo kujua kuwa wanapotazam ndipo moyo wao unakula.Hivyo wengi wamejikuta wakitamka na kutenda mambo maovu pasipokujua kuwa wao wenyewe ndio waliojitengenezea hayo mambo mioyoni mwao.Kama moyo wako unahitaji kalinda Utakatifu basi sio kila kitu kinafaa kuangaliwa na wewe,kwa maana unachokiangalia kinaweza kutia moyo wako unajisi.

Mithali 23;33
Macho yako yataona mambo mageni;Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.

Neno la msingi hapa ni mambo Mageni,Lazima mtu ajiulize Mambo mageni ni mambo ya namna gani hata yaweze kusababisha moyo wa yule anayetazama utoe mambo yaliyopotoka.
Kwa vyovyote vile mambo haya lazima yatakuwa yamepotoka na ndio maana matokeo yake ni akiba ya Uovu moyoni mwa aliyeona.
Neno la Mungu linasema(Kumbu 32;12) Wala msiabudu miungu wageni.Maana yake mambo mageni ni mambo yanayohusu miungu wageni.Maana yake mtu anapotazama vitu vyote vya mungu megini ambaye ni Ibilisi matokeo yake ni Moyo wake kutoa yaliyopotoka. Hii inakupa kuona kuwa wakati mtu anapokuwa anatazama mambo haya alikuwa anaweka akiba kwenye moyo wake akiba iliyopotoka na ndio itakuja kudhihirika baadae.Maana yake chochote anachokitazama mtu kama anayetukuzwa hapo ni mungu megeni au Ibilisi tarajia kabisa moyo wake kutoa Maovu baadaye.


Kumbukumbu 32:12
Bwana peke yake alimwongoza, Wala hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye



2.Sikio
Sikio lako ni Kinywa cha moyo wako..Ukisoma maneno ya Ayubu utashangaa kidogo kukuta maneno haya juu ya sikio,,Ayubu 12;11Je sikio haliyajaribu maneno kama Ulimi uonjavyo chakula Ulimi huonja chakula na kamwe hautakula chakula kilicho kichungu labda tu iwe ni dawa,ndivyo hivyo Sikio nalo huyajaribu maneno,Kwanini linayajaribu ? Hii ni kwasababu sio kila chakula kinafaa kwa afya ya moyo vipo vingine ni sumu na vikiruhusiwa tu kuingia basi moyo utaharibika.

Ukisoma 1Corinto 15;33..Utakutana na maneno hayaMsidanganyike;Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema..Tabia ni matunda ya hali ya moyo, hivyo njia pekee ya Mazungumzo kuweza kuharibu Tabia njema ni kama hayo mazungumzo yanaweza kuathiri asili ya mti yaani moyo.Tabia njema ni matokeo ya akiba njema iliyondani ya moyo wa mtu.Hivyo kama mtu mwema ataanza kuweka akiba mbovu ndani ya moyo wake baasi baada ya muda tabia mbaya ndiyo itakayodhihirika kwasababu mtu mwovu kutoka kwenye akiba mbovu hutoa maovu.Na Roho Mtakatifu anaonya kabisa kuwa Tusidanganyike mazungumzo mabaya huharibu tabia njema lazima tuelewe jambo hili kuwa maneno haya mabaya yanaingia kwenye moyo na baada ya muda yanaanza kudhihirika nje kwa kinywa au matendo.

Waefeso 5;3-5.inazungumza juu ya kuonya watakatifu kuwa Uasherati usitajwe kwao,yaani haiwapasi watakatifu kuwa na mazungumzo yanayohusu uasherati,,na agizo hili sio juu ya kufanya Uasherati bali ni juu ya Kuuzungumzia,baada ya kutafakari sana Roho Mtakatifu akanionyesha kwanini Alionya kuhusu Uasherati kutajwa(kuzungumzwa na watakatifu).Ukiangalia maneno hayo Utaona katazo la kutaja mambo ya Uasherati mstari wa 3 halafu mstari wa 5..anasema Maana mnajua Waasherati hawataa urithi Ufalme wa Mungu,,sasa waweza kujiuliza kwani kuzungumzia mambo ya Uasherati na Mwasherati vinamahusiano gani.Lakini Waasherati wanaotajwa mstari wa 5 wanatengenezwa na mazunguzo ya Uasherati waliyokuwa wanayataja hapo kwenye mstari wa 3 walipokuwa watakatifu.Maneno yanaumba tabia ndani ya mtu hivyo Mtakatifu akiendelea kusikiliza na kujihusisha na mazungumzo ya Uasherati baaada ya muda atakuwa mwasherati.Mazungumzo unayoyasikiliza yanakuumbaa uwe mtu wa aina ya mazungumzo unayoyasikiliza.Unaweza usione madhara mwanzoni lakini Neno la Mungu limehakikishwa baada ya muda utakuwa kama marafiki unaoombatana nao kwakusiliza mazungumzo yao.Maana wanapozungumza wewe unakula.Angalia sana watu unaoshiriki nao ni kama hotel unayokula,kama wanazungumza maneno machafu basi ujue unakula jalalani na baada ya muda uchafu utatoka kwenye moyo wako.Wapumbavu tu ndio hula jalalani.

Waefeso 5;3-5 Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru.Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi. Basi msishirikiane nao.”


Naamini umepata kitu cha kukusaidia kuulinda moyo wako.Tutaendelea Mungu akitupa Neema yake katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Amani na Neema zitokazo kwa Bwana Yesu ziwe kwako.

JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2   JINSI YA KULINDA MOYO WAKO-2  Reviewed by Unknown on 6:02:00 PM Rating: 5

3 comments:

  1. Nimebarikiwa sana ....Mungu akutie nguvu

    ReplyDelete
  2. God Bless you I am blessed

    ReplyDelete
  3. Barikiwa Maana wa Mungu,nimejifunza kiti

    ReplyDelete

Sora Templates