NAMNA YA KUKUZA NA KUIMARISHA ROHO YAKO-3
Tunaendelea na mwendelezo wa somo letu wa namna ya kukuza na kuimalisha roho yako, na sasa tunaingia jambo la pila baada ya kujifunza jambo la kwanza ambalo ni neno la Mungu. Na sasa ni kusifu na kuabudu.
Kusifu na kuabudu ni njia nyingine ambayo unaweza kuitumia kukuza
na kuimarisha roho yako. Mungu pia huitumia sana njia hii anapotaka kuimalisha
roho yako. Ikumbukwe kwamba, kama nilivyosema hapo awali, njia zote hizi
zinalenga kumkaribia Mungu, kwa sababu mtu anaimarika rohoni kwa kadiri
anavyomkaribia Mungu. Uimara rohoni ni matokeo ya ukaribu na Mungu. Kusifu na
kuabudu ni njia moja wapo iliyorahisi kumkaribia Mungu. Kwa sababu kuabudu
kunahusisha roho (ya kwako) na Roho ya Mungu kushirikiana. Kuabudu ni kuileta
roho yako kwenye makutano na Roho ya Mungu uweponi mwake.
Kabla ya kuendelea mbele zaidi ni vyema tukaelewa maana ya kusifu
na kuabudu ili tuweze kuelewa ipasavyo namna ambavyo kunaweza kukuza na
kuimarisha roho ya mtu. Kusifu na kuabudu ni maneno mawili tofauti yenye maana
tofauti pia ingawa yanatumika pamoja. Utofauti wao unatokana na kitendo chenyewe
na matokeo yake.
“Uligeuza
maombolezo yangu kuwa kucheza, ulinivua nguo za gunia ukanivika furaha, ili
moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. Ee BWANA wangu, nitakushukuru
milele.” (Zab
30:11-12)
“Nitakushukuru
milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; mbele ya
wacha Mungu wako”
(Zab 52:9)
“Haleluya,
Enyi mataifa yote, msifuni BWANA, Enyi watu wote, mhimidini. Maana fadhili zake
kwetu ni kuu, Na uaminifu wa BWANA ni wa milele” (Zab 117:1-2)
Ukiangalia mistari hii na mingine
mingi kwenye biblia unaweza ukaelewa kiurahisi maana ya kusifu. Zaburi ya 30
inasema uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza ili moyo wangu ukusifu
wewe, Zaburi ya 117 inasema enyi mataifa msifuni BWANA, kwa maana fadhiri zake ni
za milele. Kwa hiyo kusifu ni matokeo ya kile ambacho Mungu amekifanya.
Amegeuza maombolezo, amedhihirisha fadhiri zake, kwa sababu hiyo Mungu
anasifiwa. Tunamsifu Mungu kwa matendo yake makuu aliyoyatenda na kuyafunua.
Kwa ujumla tunaweza kusema;
Kusifu
ni mwitikio wa moyo wa mtu kwa yale ambayo Mungu ameyatenda. Ni kukiri na
kutangaza yale ambayo Mungu ameyafanya.
Mwitikio ni matokeo ya moyo
kutambua (Recognize) yale ambayo Mungu ameyafanya iwe ni kwake au mtu mwingine.
Sifa za Daudi, Asafu na wanawe, Yeduthuni na wanawe zilikuwa ni matokeo ya
mambo ambayo Mungu alitenda kwao na katikati ya Israeli. Daudi anaposifu uweza
wa Mungu kuokoa na mauti, ni kwa sababu aliona jinsi alivyomuokoa na mauti
kutoka mkono wa Sauli na adui zake wengine. Hatusifu kwa sababu eti tunajisikia
kufanya hivyo, hapana ila ni matokeo ya ufahamu ulioingia moyoni kwamba hakika
kilichofanyika ni mkono wa Mungu kiasi ambacho moyo wake hauwezi kutulia. Daudi
anasema,”….. ili moyo wangu uweze
kukusifu na usikae kimya…..” Zab 30:11-12). Moyo unashindwa kutulia ni kwa sababu ya kutambua kile ambacho
Mungu amekifanya mishani mwako au kwa watu wengine. Hatusifu kwa sababu tu
tumeambiwa na kusikia tu bali kwa sababu mioyo yetu inatambua na kudhibitisha
hayo matendo makuu ya Mungu. When our hearts realize what God has done, praises
flow out of us. Unapoona mtu anapoambiwa huu ni mda wa kumsifu Mungu, tuwapo
sehemu za ibada, lakini hajali, ni udhihirisho wa kwamba moyo wake hautambui
mambo ambayo Mungu ameyafanya hata kama ameyasikia hayo.
“Ndipo Yesu akaanza
kuilaumu miji ambamo alifanya miujiza yake mingi kuliko kwingine, kwa maana
watu wake hawakutubu. “Ole wako,
Korazini! Ole wako Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu,
ingelifanyika Tiro na Sidoni, miji hiyo ingekuwa imetubu tangu zamani kwa kuvaa
magunia na kujipaka majivu”.
(Math 11:20-21)
Miji ya korazini na Bethsaida ilikuwa
ni baadhi ya miji iliyo kushuhudia matendo makuu ya Mungu kwa ishara na miujiza
kupitia mwanae Yesu Kristo lakini mioyo yao isiweze kutambua. Their heart never
recognized and realized God’s doings in their midist, and thus didn’t turn back
to God. Realizing, everytime God does His work, it is a sign that you are
spiritually alive. Most of the time when God does anything, He intends to
awaken your spirit (heart)- bringing it to it’s original sense. Hiki ndicho
alichokuwa anajaribu kufanya kwa miji ya korazini na Bethsaida, mioyo yao iweze
kuamka na kutambua kinachofanyika ile iweze kumrudia Mungu.
Nazungumza kwa habari ya moyo
(roho) wako. Kama moyo wako hauwezi kutambua kile ambacho Mungu amekifanya, kusifu
kwako hakuna nguvu- your praises has no power, it loose it’s meaning. Mioyo
yetu inapokosa ufahamu juu ya kile ambacho Mungu amefanya hata kama tumesikia,
kusifu kwako kunakosa maana kwa sababu hiyo kunakosa nguvu. Kwa mfano,
tunaposhindwa kutambua jinsi Mungu alivyomfufua Yesu toka kwa wafu kwa uweza wa
Roho wake mtakatifu, hata kama tumesikia, sifa zetu hazina maana kwa sababu
hiyo zinakosa nguvu. Kwa sababu hatuwezi kumsifu Mungu kwa maneno tu alafu
mioyo yetu iko mbali. Daudi anasema. ,”…..
ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya…..”. kusifu kunakuwa na maana
na nguvu kunapokuwa ni matokeo ya moyo kushindwa kutulia kwa sababu ya kile
ambacho Mungu amekifanya.
“Basi Waisraeli
walipoona uwezo mkubwa BWANA aliodhihirisha dhidi ya Wamisri, watu wakamwogopa
BWANA na wakaweka tumaini lao kwake na kwa Musa mtumishi wake. Ndipo Musa na Waisraeli
wakamwimbia BWANA wimbo huu: “Nitamwimbia BWANA, kwa kuwa ametukuka sana.
Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini. BWANA ni nguvu zangu na wimbo
wangu, amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu, Mungu wa baba
yangu, nami nitamtukuza. …..Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni, akatwaa
tari mkononi mwake na wanawake wote wakamfuata na matari yao wakicheza. Miriamu
akawaitikia ‘‘Mwimbieni BWANA, kwa maana ametukuka sana. Farasi na mpanda
farasi amewatupa baharini”
(Kut 14:31, 15:1, 20-21)
Waisraeli walipoona uweza mkubwa
ambao BWANA aliufanya katikati yao waliingiwa na hofu ya kumuheshimu Mungu- ile
hofu ni uthibitisho ya kwamba mioyo yao imetambua na kukubali kile ambacho Mungu
alikifanya kiasi ambacho walishindwa kujizuia, wakaanza kumwimbia Mungu kwa
kuyakiri na kuyatangaza yale matendo makuu. Mioyo ilikuwa kama vile karibia
inapasuka kiasi ambacho wanawake wa waisraeli walishindwa kujizuia. Miriamu
pamoja na wanawake wote wakajipanga pamoja kwa matari na kuimba na kucheza. Why
all the praises and the dances? Kwa sababu mioyo yao ilishindwa kutulia kwa
kile ambacho Mungu amekifanya katikati yao. Kuimba na kucheza ilikuwa ni
mwitikio wa roho zao. Kuimba na kucheza kunapokuwa ni mwitikio wa roho yako,
hakuna kinachoweza kukuzuia. Hakuna sababu yoyote itakayoweza kukuzuia usimsifu
na kumchezea Mungu. Maumivu, magonjwa, aibu, cheo n.k, vyote hivi haviwezi
kukuzuia. Kwa sababu hiyo Mungu anakuwa kiini cha sifa zako.
“Kwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu katika kusanyiko kubwa,
nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wakuchao wewe” (Zab 22:25)
Sipati picha jinsi ambavyo kanisa
lingekuwa linalipuka kwa sifa na kucheza namna hii. Lakini kilicho kibaya zaidi
ni kwamba mataifa wanaweza wakatambua matendo makuu mioyoni mwao kuliko hata
watu wa Mungu, ndio maana hata mataifa wwanaweza kumsifu Mungu. Wakati
waisraeli wanalalamika kwamba Musa amesabisha mateso yao yaongezeke, ni wakati
huo huo waganga wanamwambia Farao hakika hiki ni chanda cha Mungu katika jambo
ambalo Mungu alilifanya. Mungu alitazamia watu wake wangekuwa mstari wa mbele
kuyatangaza matendo yake- ndiyo kuyatangaza, kwa sababu kusifu ni kuyatangaza
na kuyakiri matendo makuu ya Mungu. Mtu anapokuwa kimya asifanye jambo lolote,
hawezi kusifiwa lakini anapofanya jambo, hujidhirisha kwa watu, na sifa zake
husambaa na kwenda mbali kwa kutangazwa na watu. Na Mungu hivyo hivyo
anapojifunua kwa matendo yake, anatarajia watu wake wayakiri na kuyatangaza kwa
mataifa ndio maana Daudi anasema,
“Mwimbieni BWANA
sifa, ametawazwa Sayuni, tangazeni miongoni mwa mataifa yale aliyoyatenda” (Zab 9:11)
Haleluya!
Kusifu kunamfanya Mungu aweze
kuyaachilia yale mambo aliyoyakusudia maishani mwa mtu. Kusifu kunatngeza
mazingira ya Mungu kuenda mahali pake kwa ajili yako na kufanya aachilie nguvu
zake. Katika soma yangu biblia nikagungua Mungu huketi sehemu mbili tu, juu ya
kiti chake cha enzi na juu ya sifa za watu wake. Kwa hiyo sifa zinageuzwa kuwa
mahali pa kuketi pa Mungu. Kwa sababu sifa zinapotangazwa zinambeba Mungu kwa
heshima yake ile ile. Ni muhimu kutangaza sifa za Mungu kwa ajili ya Mungu na
kwa ajili yetu pia. Kwa Mungu jina lake linasambaa, na kwetu ni wokovu.
Kuabudu. Baada ya kuchambua kidogo kuhusu
kusifu, ni vyema tunaangalia pia kuabudu. Kuabudu ni tofauti na kusifu kwa
sababu kuabudu kupo kiundani sana kuliko kusifu (worship is more deeper that
praise) kwa maana kwamba kuabudu inahusu Mungu ni nani na wewe ni nani (Worship
is about who God is and who you are). Kuabudu inahitaji uelewa wa Mungu ni nani
na wewe ni nani (worship requires understanding who God is and understanding
who you are). Haihusiani na kitu ambacho Mungu amekifanya bali jinsi alivyo.
Lakini wengi tunabubu Mungu tusiyemjua vizuri. Yesu alimtahadharisha yule
mwanamke msamalia akisema
“Ninyi Wasamaria
mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi
tunamwabudu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi” (Yoh 4:22)
Wasamalia walikuwa wanaabudu
Mungu wasiyemjua lakini wayahudi walimwabudu Mungu waliyemjua. Ndivyo
itupasavyo kumwabudu Mungu tunayemjua. Ndio maana Paulo aliamua kuwasaidia watu
wa Athene walipokuwa wanaabudu Mungu wasiyemjua ili waweze kumjua.
“Ndipo Paulo akasimama katikati ya
Areopago akasema, “Enyi watu wa Athene! Ninaona kwamba katika kila jambo ninyi
ni watu wa dini sana. Kwa kuwa nilipokuwa nikitembea mjini na kuangalia kwa
bidii vitu vyenu vya kuabudiwa, niliona huko madhabahu moja iliyoandikwa: KWA
MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi sasa kile ambacho mmekuwa mkikiabudu kama
kisichojulikana, ndicho ninachowahubiria” (Matendo 17:22-23)
Kuabudu
kuna msingi katika kumjua na kuelewa Mungu ni nani, asili yake na tabia zake. Paulo
akaamua kuwasaidia kuelewa na kupata ufahamu juu ya Mungu wasiyemjua, ili
wasifanye makosa tena kuabudu Mungu wasiyemjua. Ebu tuangalie kwa pamoja mstari
ambao utaweza kutusaidia vizuri kuelewa kuhusu kuabudu.
“Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo
wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu
namna hii, ndio Baba anawatafuta” (Yoh 4:23)
“A time will come, however, indeed it is
already here, when the true (genuine) worshipers will worship the Father in
Spirit and in truth (reality), for the father is seeking just such people as
these as His worshipers” (John 4:23 AMP)
Kuna
mambo kadhaa tunayoyaona kwenye huu mstari:-
1. 1. Kuna
waabuduo halisi na wasio halisi,
Tofauti
ya waabuduo halisi (genuine) na wasio halisi inakuja wakati wa kuabudu- kuabudu
katika roho na kweli. Roho hapa inazungumziwa habari ya roho yako, na kweli
hapa, kwenye biblia ya tafsiri ya kiingereza imeweka kwenye mabano neno reality
ikiwa na maana ya uhalisia. Kwa hiyo waabuduo halisi watamwabudu BABA kwa roho
zao lakini katika uhalisia wa BABA jinsi alivyo. Sababu ya kumwabudu Mungu
katika roho ni kwa sababu yeye ni Roho (Yoh 4:24). Ni vyema kuelewa kwamba Mungu
anatafuta roho zinazoweza kumwabudu yeye katika uhalisia wake. Roho zetu
zinapata kuujua uhalisia wa Mungu jinsi alivyo kwa njia ya ufunuo katika neno
lake kupitia Roho wake mtakatifu. Ufunuo unaoupata ndio unaokusukuma kumwabudu
Mungu. Sababu inayowafanya wazee Ishirini na nne, wenye uhai wane na malaika
wamwabudu Mungu bila kukoma ni kwa sababu wanamuona Mungu kwa uhalisia wake
wote bila kipimo, utukufu wake wote na enzi yake yote.
“Pia kukizunguka
hicho kiti cha enzi palikuwa na viti ishirini na vinne na juu ya hivyo viti
walikuwa wameketi wazee ishirini na wanne, waliovaa majoho meupe, wakiwa na
taji za dhahabu vichwani mwao. Kwenye kile kiti cha enzi palikuwa panatoka
miali ya umeme wa radi, ngurumo na sauti za radi. Mbele ya hicho kiti cha enzi,
palikuwa na taa saba zilizokuwa zinawaka. Hizi ndizo Roho saba za Mungu. Pia
mbele ya hicho kiti cha enzi palikuwa na kile kilichoonekana kama bahari ya
kioo, iliyokuwa angavu kama jiwe lisilo na rangi yo yote ling’aalo sana……Kila
mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na
macho pande zote, hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kusema:
‘‘Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako,
aliyeko na atakayekuja.’’ Kila mara viumbe hao wenye uhai wanne walipomtukuza,
kumheshimu na kumshukuru Yeye aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, tena aishie
milele na milele, wale wazee ishirini na wanne huanguka mbele Zake Yeye
aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi na kumwabudu Yeye aliye hai milele na
milele. Wao huziweka taji zao mbele ya hicho kiti cha enzi wakisema” (Ufunuo 4:4-6, 8-10)
Hawa viumbe hai wanamuona na
kukutana Mungu uso kwa uso mahali pale walipo. Wanapoona uzuri wa Mungu ulivyo,
mngáo wa kiti cha enzi, na bahari ya kioo mbele za kiti cha enzi, ngurumo na radi
zinazotoka hapo, zinawasukuma kumwabudu Mungu. Mungu anapojifunua, inatupa
sababu ya kumwabudu. Na yeye hujifunua moyoni mwako. Yesu alimwambia mama
msamalia kwamba watu hawataenda Yerusalemu kuabudu wala katika mlima, kwa maana
huko ndiko Mungu alikuwa anajifunua lakini saa yaja ambayo ipo tayari ambayo
Mungu atajifunua mioyoni mwa watu, na kwa sababu hiyo watamwabudu katika roho
sawa sawa na ufunuo wanaoupata. Mahali
ulipo Mungu hujifunua moyo, ili uweze kumwabudu ndio maana akili wala mwili
wako hauwezi kumwabudu Mungu.
Kuabudu ni kuingia katika uwepo
wa Mungu kwa roho yako, mahali ambapo unakutana naye na kumwona alivyo. (Worship
is about getting into God’s presence by your spirit, where you meet Him and
experience His reality). Our spirits get to contact God who is Spirit in
worship with a clear demarcation of who God is and who we are. In fact it is
through worship we understand who we are. Kuabudu sio kuhusu nyimbo, kwa sababu
unaweza ukamwabudu Mungu bila wimbo. Kuna wengine ambao wanalowea kwenye nyimbo
na kuacha kiini cha kuabudu- Mungu mwenyewe. Na unaweza kufikia hapo kwa roho
yako lasivyo haiwezekani hata kama ukiimba vizuri. Wakati wa kuabudu ndio
wakati wa kukutana na nguvu za Mungu kwa sababu roho yako hukutana moja kwa
moja na Roho ya Mungu- chanzo cha nguvu. Ndio wakati ambao tunapata nafasi ya
kupokea vitu kutoka kwa Mungu ambaye ni Roho kwa roho zetu. Ni muda wa kujenga mahusiano
mazuri na Mungu kwa sababu unapata nafasi ya kuutazama na kushiriki uhalisia na
uzuri wake. Kwa sababu hiyo mtu hiimarika sana rohoni na kuwa na nguvu.
Endelea kufatilia mundelezo wa
somo hili, Mungu akubariki
NAMNA YA KUKUZA NA KUIMARISHA ROHO YAKO-3
Reviewed by Unknown
on
2:17:00 PM
Rating:

No comments: