USHIRIKA NA MUNGU KATIKA VITA
“Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu Zake” (Efeso 6:10)
Kabla ya kuanza kupigana vita ni muhimu kujiandaa vyema, ndivyo wanajeshi wanavyofanya. Na vita vya kiroho vivyo hivyo. Paulo anatuambia tuvae silaha zote za Mungu ili tuweze kupigana siku ya uovu, (Efeso 6:13).
Kwenye hivi vita vya kiroho kabla ya kuvaa silaha hizo kitu cha msingi Paulo anakitaja ni kwamba, mzidi kuwa hodari katika Bwana, akiwa na maana kwamba jengeni uhodari wenukutoka katika ushirika na BWANA, au mtaweza kuzidi kuwa hodari kama mtaimarisha ushirika na Mungu (Union with God).
Na anaongezea kwamba katika ushirika huo, uweza wa nguvu zake mtapata. Nguvu za kupigana tunazitoa kwake, Ushirika na yeye (muunguniko tulionao na yeye ndio unaotuhakikishia nguvu zake). Kukata ushirika na Mungu ni kukata na uweza wa nguvu zake pia.
Kwa hiyo kabla ya kwenda kupigana vita vya kiroho ni Muhimu kuangalia nafasi yako na uhusiano wako na Mungu kwa sababu utaweza kupata ushindi kama ukiambatana naye. Hata kama umevaa siraha zake zote lakini huna ushirika mzuri naye vita utakayoenda kupigana itakuwa ngumu kwako kwa sababu atakuwa hayupo pamoja na wewe.
Daudi alikuwa akishinda vita kwa sababu BWANA alikuwa pamoja naye, biblia inasema ”Daudi akazidi kuwa na mamlaka zaidi na zaidi, kwa sababu BWANA Mungu Mwenye Nguvu alikuwa pamoja naye” (2 Samweli 5:10). Mungu akiwa upande wako unauhakika wa kushinda. Daudi anasema “BWANA yuko upande wangu sintaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? BWANA yuko upande wangu, msaidizi wangu kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa” (Zab 118:6-7). Hii ni kwa sababu ushindi hautokani na silaha ulizovaa bali Mungu aliye pamoja nawe kwa hiyo usiamini silaha kuliko Mungu. Tengeneza uhusiano wako na Mungu kama unahitaji ushindi katika maisha yako.
USHIRIKA NA MUNGU KATIKA VITA
Reviewed by RHEMA'S VOICE MINISTRY
on
9:30:00 PM
Rating:

No comments: