SIFA KATIKA UZURI WA UTAKATIFU
2 Nyakati 20:21 "Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu...."
Duniani kunawaimbaji wazuri na wenye vipawa vikubwa sana na wanaonekana
kumsifu Mungu vizuri. Kumwimbia na kumsifu Mungu sio jambo la mtu flani
ila ni jambo la kila mmoja.
Watu
wengi hatuoni baraka za Mungu zikishuka ktk maisha yetu ama Mungu
akijidhihirisha uwepo wake wakati tunamwimbia na kumsifu kwa sababu
tumekuwa tukimsifu vizuri ila hatujajua kumwimbia na kumsifu katika
UZURI WA UTAKATIFU wake.... Hadi pale tutakapo ijua siri hii na
kujifunza kumwimbia na kumsifu katika UZURI WA UTAKATIFU ndipo tutakapo
muona Mungu akijidhihirisha!
Omba Roho Mtakatifu akufundishe jinsi ya kumsifu Mungu katika UZURI WA UTAKATIFU ili uzione baraka katika sifa.
Maandiko yanasema "....akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu..."
Mfalme hakuangalia nani anayejua kuimba na kumsifu Mungu maana naamini
aliamini kuwa kila mtu anajua kumwimbia na kumsifu Mungu lakini alienda
mbali zaidi i.e ili ashinde vita ni lazima awaweke watu wanaoijua siri
iliyopo katika kusifu nao watamwimbia na kumsifu katika UZURI WA
UTAKATIFU ili waweze kutangulia mbele ya jeshi kuhakikisha kuwa ushindi
unapatikana kwa njia ya kumwimbia na kumsifu MUNGU kama alivyokuwa
amewaambia.
Mungu akufundishe kumsifu YEYE maana ni zaidi ya kurukaruka, kukariri nyimbo na kutamka maneno.
SIFA KATIKA UZURI WA UTAKATIFU
Reviewed by RHEMA'S VOICE MINISTRY
on
3:12:00 AM
Rating:

No comments: