BREAKING NEWS

[5]

KUNA NGUVU KATIKA KUTULIA

ISAYA 30;15 ''Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa;Nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumainia, lakini hamkukubali''

Maamuzi yoyote yanayofanywa na mtu yanategemea sana hali ya ndani.Kufanya maamuzi sahihi au mabaya kote kunategemea aliyefanya maamuzi alifanya akiwa na hali gani ndani ya nafsi yake.Mungu kwa kutambua hili anamsemesha mwanadamu kuhusu kutulia na kutumainia maana katika kutulia ndipo atakapopata nguvu na hekima sahihi ya kufanya maamuzi,lakini inaonekana mwanadamu Hajakubaliana na Mungu katika hili ndio maana Mungu anasema ''lakini hamkukubali''


Hebu tutazame pamoja madhara ya Kutokutulia na kutumainia
Natamani kuongelea sehemu ambayo inasumbua kanisa hasa Vijana.
Ni jambo lililowazi kuwa kuwa moja ya kitu kinachovuruga hali ya Utulivu wa ndani wa Vijana ni kuachwa au mahusiano kuvunjika.
 

Inapotokea wawili wameachana ndani ya nafsi zao huwa kuna jeraha ambalo huondoa kabisa utulivu wa ndani
 

Hali ya huzuni na Upweke huwakumba wengi.Hali hii ya upweke hupelekea wengi Kukimbilia kwenye mahusiano mengine hasa wadada wakijaribu kutuliza hali ya upweke uliozikumba nafsi zao.

Lakini majira haya ni majira ambayo Mtu anapaswa kutulia na Kutumainia na nguvu za mtu kama huyu zinakuwa katika Kutulia.
 

Ukweli ni kwamba katika mazingira kama haya mtu anakuwa hana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwasababu kinachomsukuma sio wakati wala kusudi ila Njaa iliyopo kwenye nafsi yake.
 

Mithali 27;7b ''Bali nafsi yenye njaa huona kitu kichungu kuwa kitamu''
 

Maana wakati kama huu kwasababu ya Upweke mkubwa unaosumbua nafsi mtu hawezi kupima tena yule anayeingia naye kwenye mahusiano mapya maana neno linasema katika njaa hata kichungu huonekana kitamu,hata kama unayeingia naye kwenye mahusiano mapya sio sahihi hutaweza kuona maana umefumbwa macho na njaa yako.

Yesu alipokuwa jangwani na njaa ikampata shetani aliona ndio wakati sahihi wa kumjaribu,ambacho hakunote shetani ni kuwa ''Jesus was hungry but he was not desperate''.na hivyo hakusukumwa kufanya maamuzi na njaa yake.Angekuwa desparete angegeuza jiwe kuwa mkate,lakini alitulia na kulitazama neno la Mungu na kumshinda shetani.

Usiruhusu njaa yako ikufanye ugeuze jiwe kuwa mkate nawakati unachohitaji ni Neno na sio mkate.
 

Usigeuze mwanaume/mwanamke yoyote kuwa wa kwako kwasababu ya njaa yako.
Tulia maana neno linasema Nguvu zako zitakuwa katika Kutulia.
KUNA NGUVU KATIKA KUTULIA KUNA NGUVU KATIKA KUTULIA Reviewed by RHEMA'S VOICE MINISTRY on 3:21:00 AM Rating: 5

No comments:

Sora Templates