BREAKING NEWS

[5]

KUTEMBEA KATIKA ROHO-2



 KUTEMBEA KATIKA ROHO-2

Bwana Yesu asifiwe sana mwana wa Mungu..!!
Karibu sana tuendelee na sehemu ya pili ya Mwendelezo wa somo letu la KUTEMBEA KATIKA ROHO,kama hukupata nafasi ya kupitia sehemu ya kwanza,unaweza kulipata kwenye blog yetu ya rhemavoice.blogspot.com au kwenye page yetu ya facebook-Rhemas Voice Ministry.
Sehemu ya kwanza tulishia kwenye kuona Tabia za Roho Mtakatifu na Karama za Roho Mtakatifu.Leo tuanzia hapo hapo kwenye tabia za Roho Mtakatifu.

Tabia ya Roho Mtakatifu ni ya msingi sana kuliko Karama kwasababu kutembea kwako kwenye karama kutatunzwa na tabia za Roho Mtakatifu ndani yako.Karama haiwezi kukulinda na dhambi bali Tunda la Roho Mtakatifu.Ukifanikiwa kuwa na Karama kubwa halafu hujafanikiwa kutembea katika matunda ya Roho Mtakatifu kuna hatari kubwa hiyo karama ikawa chanzo cha anguko lako.Si maanishi kuwa Karama sio kitu cha msingi la hasha,ni Kitu cha msingi ni kitendea kazi unachokihitaji ili uweze kusimama kwenye ofisi uliyoitwa,lakini Tabia,Tabia ndio itakayokulinda,ndiyo itakayokupeleka mbali katika safari ya Ofisi yako.

Tuangalie baadhi ya Watumishi wa Mungu waliokuwa wakubwa sana kwenye Biblia,waliokuwa na Karama nyingi na za kutisha lakini kwasababu ya kushindwa kutembea kwenye tabia za Roho Mtakatifu kuna viwango hawakufikia,kuna mashambulizi walipata kutoka kwa adui na hata wengine kuwa na mwisho mbaya.

Musa
Musa ni moja ya watumsh wakubwa sana waliowahi kutembea na Mungu na kutembea katika uweza wa ajabu wa Roho Mtakatifu.
Lakini pamoja na yote kuna kiwango Musa hakufikia,alipaswa kufika Kaanani lakini hakuingia na ukichinguza maandiko utakuja kuona kuwa Kushindwa kutembea katika Tabia/tunda la Roho Mtakatifu ndio iliyomgharimu.

Hesabu 20:2-12

2 Na hapo hapakuwa na maji kwa ule mkutano; wakajikusanya juu ya Musa na juu ya Haruni.

 3 Watu wakashindana na Musa, wakanena, wakisema, Ingalikuwa heri kama tungalikufa wakati ule ndugu zetu walipokufa mbele za Bwana!

 4 Mbona mmewaleta kusanyiko la Bwana hata jangwa hili ili tufe huku, sisi na wanyama wetu?

 5 Na mbona mmetupandisha kutoka Misri ili kutuleta hata mahali hapa pabaya? Si mahali pa mbegu, wala tini, wala mizabibu, wala makomamanga; wala hapana maji ya kunywa.

 6 Musa na Haruni wakatoka pale palipokuwa mkutano, wakaenda hata mlangoni pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa Bwana ukawatokea.

7 Bwana akasema na Musa, akinena,

 8 Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao.

 9 Musa akaitwaa hiyo fimbo kutoka mbele za Bwana kama alivyomwamuru.

 10 Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu?

 11 Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia.

 12 Bwana akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa.

Ukisoma maandiko haya utaona jinsi kusanyiko lilivyomshambulia Mtmsh wa Mungu Musa hata kusababisha ashindwe kufuata maelekezo aliyopewa na Mungu.Kwenye Mstari wa 12 Utaona Mungu akisema Musa na Haruni hawakumwamini kwa kutokufuata maelekezo yake. Lakini ukienda kwenye Zaburi utagundua kulikuwa kuna kitu zaidi kilichomfanya Musa akatenda vile mbele za Bwana na kupewa adhabu ya kutokufika Kaanani.

Tazama haya maneno ya Musa kwa umakini kuna kitu utakiona ndani ya Musa.
……Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu?

 11 Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia.

Utaona ndani ya haya Maneno ya Musa kulikuwa kuna hasira ndani yake.Kutokana jinsi hawa jamaa walivyomsumbua nafsi yake.
Zaburi 106:32-33

32 Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba, Hasara ikampata Musa kwa ajili yao,

 33 Kwa sababu waliiasi roho yake, Akasema yasiyofaa kwa midomo yake.
Ukisoma kwenye biblia ya kingereza huu mstari wa 33 unasomeka hivi
Because they provoked his spirit, so that he spake unadvisedly with his lips.(KJV)

They made him bitter so that he spoke recklessly.(NSB)
Utaona hapa Musa alikasirishwa sana nay ale manunguniko ya Wanaisrael na matokeo yake katika hasira alisema yasiyofaa na gharama yake ilikuwa kubwa sana.
Hasira ndiyo iiyomgharimu,Palipohitajika Tunda la Uvumilivu hasira ikatawala ndani yake. Utaona kuwa Karama alikuwa nayo ya Miujiza ya Ajabu lakani hakushughulikia hasira yake na ilimgharimu.Hasira ya haraka,ya kulipuka,isiyoweza kutawaliwa ni tunda la mwili ambalo kama hujachukua hatua kulishulikia litakukwamisha maeneno mengi sana katika Kutembea kwako na Mungu.

Ukichunguza kwa makini utagungua hasira ya Musa haikuwa hasira ya kawaida tu,ilikuwa ni hasira ya Laana.
Musa ni mwana wa Lawi,na Hasira ya Baba yake Lawi ililaaniwa na Babu yao Mzee Yakobo.Kwa hiyo kulikuwa mlango wa adui kupita na kumvuruga Musa kupitia Hasira.

Mwanzo 49:5-7

5 Simeoni na Lawi ni ndugu; Panga zao ni silaha za jeuri.

 6 Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe;

 7 Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.

Sasa unaweza kuona chimbuko la ile Hasira ya Musa.Kuna watu wana hasira za kawaida na kunawengine ni roho,inasukumwa na nguvu ya giza ndani yake.Kwa Musa ilikuwa laana.Kuna watu wanahasira za Kurithi,kwenye nyumba za Baba zao hasira kali ndio asili yao.Kitu kama hii bila kuishughulikia kwa Msaada wa Roho Mtakatifu itakuharibia mambo mengi.
Mithali 16;32
 Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.

Hasira ni tabia ya Mungu ndani ya mtu,lakini Mungu sio mwepesi wa hasira.Hivyo wana wake wanapaswa kutokuwa Wepese wa Hasira.Unapaswa kuwa na uwezo wa Kuitawala hasira yako Mwana wa Mungu.Huwezi kuwa Shujaa kama hujui kuitawala hasira yako.
Kutoka 34;6

6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;

Yakobo 1;19

Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si

mwepesi wa kusema; wala kukasirika;

Unaweza kujitetea ndivyo nilivyo na utaendelea kubaki hivyo mpaka utakapokubali kuwa hiyo hasira ya haraka hivyo sio Tunda la Roho Mtakatifu bali tunda la mwili na hapo utaanza kushirikiana na Roho Mtakatifu katika kuitawala hasira yako ili isikuletee madhara maana ni hakika itaharibu nafsi yako,mahusiano yako na watu na hata kutembea kwako katika Karama za Roho Mtakatifu.

Jipime Yakobo anasema mpole wa kunena na kukasirika bali mwepesi wa kusikiliza,ndivyo ilivyokwako au kwako utaratibu umegeuka,yaani wewe ni mwepesi wa kukasirika na kuongea na sio mwepesi kusikiliza.Upole ni Tunda la Roho,Uvumilivu ni Tunda la Roho kutembea katika hayo ni kutembea katika Roho Mtakatifu.Kusudia kukua katika Uvumilivu na Upole.

Kwa leo tuishie hapo mtu wa Mungu,tutaendelea kwa kadiri Mungu atakavyotupa Neema yake.
Barikiwa sana kwa Jina la Yesu Kristo
KUTEMBEA KATIKA ROHO-2 KUTEMBEA KATIKA ROHO-2 Reviewed by Unknown on 8:18:00 PM Rating: 5

No comments:

Sora Templates