UHUSIANO KATI YA ROHO MTAKATIFU,ROHO YAKO NA FIKRA ZAKO
"Maana
ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu
iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila
Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye
kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu."
Mungu anamwongoza mwanadamu na kuwasiliana na mwanadamu kupitia Roho mtakatifu,ambaye yupo ndani yetu.
Mungu anamwongoza mwanadamu na kuwasiliana na mwanadamu kupitia Roho mtakatifu,ambaye yupo ndani yetu.
Kuna uhusiano mkubwa uliopo Kati ya
roho Mtakatifu,Roho yako na Fikra zako,Ukielewa uhusiano wa vitu hivi
vitatu itakusaidia kumsikia Mungu ambaye anatumia vitu hivi kuleta
taarifa kwako.
Hakuna ayajuaye mawazo ya moyo wa mtu ila Roho yake, vivyo hivyo hakuna Ajuaye mawazo ya moyo wa Mungu ila Roho wa Mungu,,
Roho wa Mungu anakaa ndani ya Roho zetu na yeye ndiye anayeyafunua
mawazo ya Mungu kwetu (maandiko yanasema mambo ambayo jicho halijayaaona
wala sikio halijayasikia ambayo Mungu amewaandalia wampendao)
1Corinto2;9..
Roho wa Mungu anayafunua kwenye Roho zetu, na Roho
zetu zinayaachilia kwenye Fikra zetu,..Kwa maana huwezi kuyajua
aliyokukirimia Mungu isipokuwa Roho wake amekufunulia maana yeye peke
yake ndiye anayeyajua.(1corinto2;12)
Paulo anasema(1Corinto 14;14-15)nitaomba kwa Roho(Kunena kwa Lugha) na
nitaomba kwa akili pia(Ufahamu uliyoja Neno),lakini utamsikia akiendelea
kwa kusema nikiomba kwa Roho akili yangu(Fikra) zangu Hazina Matunda
maana ufahamu haulewi nachoomba isipokuwa Roho mtakatifu anayeomba
pamoja na Roho yangu, Lakini wakati mwingine Roho mtakatifu anaweza
kuomba na Roho yako halafu ghafula unapata ufahamu fulani (kwenye
Fikra)kwamba Mungu anataka niombee jambo fulani.Huu ni moja ya mfano
unaonyesha jinsi hivi vitu vitatu vinavyofanya kazi kwa pamoja.
Mara nyingi watu wamemuuliza Mungu mambo fulani lakini hawajapata
majibu, sasa haimanishi Mungu hajajibu, wakati mwingine tayari
ameshajibu lakini kwasababu ndani ya moyo wako kuna kelele nyingi kiasi
ambacho huwezi kumsikia.
Na nikwambie tu Ukweli,,ni rahisi kunyamazisha kelele za mdomo kuliko kunyamazisha kelele ndani ya moyo wako.
Tengeneza Mazingira ya "calmness in your Mind so that you may be able to hear what God is telling you thro his Spirit"...
If there is a lot of noises in Your mind then you will miss it.
UHUSIANO KATI YA ROHO MTAKATIFU,ROHO YAKO NA FIKRA ZAKO
Reviewed by RHEMA'S VOICE MINISTRY
on
2:02:00 AM
Rating:

No comments: