BREAKING NEWS

[5]

CHOMBO CHA REHEMA

WARUMI 9;23-24
''tena, ili audhihirishe wingi wa UTUKUFU wake katika vile vyombo vya REHEMA alivyovitengeneza tangu zamani vipate UTUKUFU,NDIO SISI aliotuita...''

Ufanisi wa kazi hutegemea Ubora wa chombo au vyombo vinavyotumika kufanya kazi hiyo.Tangu mwanzo Mungu amemuumba mwanadamu ili kwa kupitia mwanadamu audhihirishe Utukufu wake.Maisha yako yamekusudiwa kudhihirisha UTUKUFU wa Mungu juu ya nchi.

Kwa maana hiyo twaweza kusema Mwanadamu ni chombo kilichoumbwa kwa kusudi la kuudhihirisha Utukufu wa Mungu,lakini ili chombo hicho kifanikiwe kinategemea sana Neema ya Mungu kwa maana kwa uweza na nguvu za kibinadamu hakuna mwanadamu awezaye kuishi maisha yanayoufunua UKUU wa Mungu kwa kiwango kile alichokikusudia Mungu.Mtume Paulo anasema katika Warumi 9;16..''si katika uwezo wa yule atakaye,wala wa yule apigaye mbio,bali wa yule arehemuye, yaani Mungu''

Maneno haya yanatuonyeshwa wazi kuwa kufanikiwa kwa mwanadamu katika kuudhihirisha UTUKUFU wa Mungu kunategemea REHEMA ya Mungu.
 

Tukiangalia vizuri sasa hapo kwenye mstari wa 23 na 23,Neno la Mungu linasema kuwa Sisi ni vyombo na si vyombo tu bali vyombo vya Rehema,na Tumetengenezwa kwa njia hiyo makusudi kabisa ili Tuweze kuudhihirisha Utukufu wa Mungu.

Mungu alipokuita kuifanya kazi yake tayari alishaachilia Tangu zamani Rehema juu yako ili ikuwezeshe kuudhihirisha UTUKUFU wake kwa viwango vya juu kabisa,
CHOMBO CHA REHEMA CHOMBO CHA REHEMA Reviewed by RHEMA'S VOICE MINISTRY on 3:39:00 AM Rating: 5

No comments:

Sora Templates